Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » SHULE YA SEKONDARI MPUNGUZI YAPOKEA MSAADA KUTOKA KWA AHMADIYYA.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Na Peter Mkwavila Dodoma.
 
JUMUIYA ya kiislamu ya Ahmadiyya Tanzania imetoa msaada wa kilo 500 za unga,sukari,maharage,na chumvi kwa shule ya sekondari Mpunguzi iliyopo mkoani Dodoma kutokana na kuathiriwa na mvua ya mafuriko iliyoambatana na upepo mkali.

Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo Sheikh wa kanda ya kati wa Jumuiya hiyo Bashart Ur Rehman Batt msaada huo umetolewa kuunga mkono wito wa serikali inayohimiza mashirika,taasisi,na watu binafsi kutoa misaada kwa jamii yenye uhitaji.

“Jumuiya ya Ahmadiyya ni moja ya sehemu inayojihusisha na utoaji wa misaada mbalimbali ikiwemo ya kiafya,kielimu na kijamii kwa kuwafikia watu wenye uhitaji kama wanafunzi hawa wa shule ya Mpunguzi”alisema.

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Esther Milang’tone aliomba mashirika na taasisi zingine yakiwemo madhehebu ya dini kuelekeza misaada katika shule hiyo ambayo imekutwa na maafa ya mafuriko na kuharibu miundombinu ya shule hiyo.

 “Ni kweli tulipata mafuriko na asilimia kubwa ya miundo mbinu ya shule hiyo iliharibiwa ikiwemo chakula na vifaa mbalimbali vya wanafunzi vilisombwa na maji”alisema.

Wakizungumza wanafunzi wa shule hiyo kwa niaba ya wenzao Zipora Elisha na Kelvin Ludovic walisema walikuwa wanashindwa kuingia madarasani kutokana na ukosefu wa chakula,hivyo kupatikana kwa msaada huo wana uhakika wa kufanya vizuri kwenye taaluma.

“Tunaishukuru taasisi ya Ahmadiyya kwa kutuwezesha msaada wa chakula tunapenda kuhakikisha kuwa tutasoma kwa umakini kwa kuwa tatizo la njaa shuleni hapo litakuwa limepungua”alisema.

Naye mkuu wa wilaya ya Dodoma Dr Jasmini Tisekwa alisema anaishukuru taasisi hiyo kwa kuunga mkono jitihada za serikali pindi yanapotokea maafa mbalimbali.

 Imeandaliwa na peter mkwavila

Mhariri: Denice J Kazenzele

 Januari/27/2016

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / SHULE YA SEKONDARI MPUNGUZI YAPOKEA MSAADA KUTOKA KWA AHMADIYYA.

No comments :