Wajumbe wanaoshiriki katika mazungumzo ya kujadili mgogoro wa kisiasa wa Burundi yanayoendelea jijini Arusha wameitaka jumuiya ya Afrika mashariki kuziba mianya inayotumika kupitisha silaha kwani asilimia kubwa ndizo zinazotumika kuangamiza watu wasio na hatia nchini Burundi.
Wakizungumza katika kikao kinachoendelea jijini Arusha baadhi ya wajumbe hao wamesema wamepata taarifa za kuwepo kwa silaha haramu zinazotumika kuangamiza wananchi wasio na hatia nchini Burundi zinazoingizwa kupitia kwenye baadhi ya bandari ikiwemo ya Dar es Saalam.
Aidha wamesema wana mategemeo makubwa na serikali za Tanzania na Kenya katika kufanikisha upatikanaji wa suluhu nchini Burundi na pia wameiomba kuyafanyika kazi madai ya upitishaji wa silaha hasa ikizingatiwa kuwa asilimia kubwa ya mizigo inayoingia nchini Burundi inapitia katika bandari za Dar es Saalam na Mombasa.
Baada ya mjadala mkali mwenyekiti wa kamati hiyo Bw. Abdulah Mwinyi pamoja na kuwataka wajumbe kuthibitisha ukweli wa madai hayo ameendelea kusisitiza kuwa hoja zote zilizotolewa zitafanyiwa kazi na vikao vya ngazi zinazohusika kikiwemo cha bunge, baraza la mawaziri na cha wakuu wa nchi wanachama.
No comments
Post a Comment