Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » LICHA YA KUKABILIWA NA NJAA ,MWENYEKITI KIJIJI CHA MATONGORO WILAYANI KONGWA ADAIWA KUUZA CHAKULA CHA MSAADA
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Na John Banda

BAADHI ya wakazi wa Kijiji cha Matongoro wilayani Kongwa mkoani dodoma wamelalamikia kitendo cha mwenyekiti wa kijiji hicho Moses Daudi kuuza chakula cha msaada ilihali wao wanakabiliwa na njaa.

Wakizungumza na a wapo redio kijijini hapo wakazi hao walidai kuwa kitendo hicho ni cha kifisadi kwa viongozi wa serikali ya kijiji kuingiwa na tamaa hivyo ni vyema wakachukuliwa hatua za kisheria.

Mmoja wa wakazi hao Ndonye Chedego alisema kuwa walipata taarifa ya kuwepo kwa chakula cha msaada gunia 59 ambazo zilipelekwa kijijini kwaajili ya vikongwe na walemavu 

Alisema kuwa Kamati ya maafa ilishirikishwa kuhusiana na kuletwa kwa chakula hicho ndipo chakula kikaanza kugawiwa juzi asubuhi kwa watu ambao walishapata chakula hicho awamu iliyopita.

Utaratibu wa ugawaji wa chakula cha msaada hapa kijijini kwetu ulikiukwa lakini jambo la kushangaza ni baada ya kuwabaini watu wana magunia ya mahindi kitu ambacho kilitushtua sana.

Aidha aliema kuwa walishangaa kukuta baadhi ya wakazi wenzao wakiwa na  magunia ya mahindi ndipo wakawabana wakazi hao na kueleza kuwa wameuziwa na Mwenyekiti wa kijiji pamoja na mtendaji.

Kwakweli tunaiomba Serikali iingilie kati suala hili  kwani tumekuwa tunateseka na njaa na hatuna uwezo

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho,Moses Daud alipoulizwa kuhusiana na suala hilo la kutuhumiwa kuuza chakula cha msaada alikataa kuwa sio kweli bali mtendaji aliuza mahindi gunia nne tu kwakushirikiana na kamati ya maafa  ili kulipia nauli ya gari ambayo ilibeba mahindi hayo.

kwa upande wake mkulugenzi mtendajiwa wa halimashauri ya wilaya ya kongwa amesema hawezi kuongea na mwandishiwa habari  kwa njia ya simu hadi afike ofisini kwake.

Imeandaliwa na John Banda

Imehaririwa na Denice J Kazenzele

january/26/2016 {jumanne}

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / LICHA YA KUKABILIWA NA NJAA ,MWENYEKITI KIJIJI CHA MATONGORO WILAYANI KONGWA ADAIWA KUUZA CHAKULA CHA MSAADA

No comments :