Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » MPANGO WA ELIMU BURE BADO NI MZIGO KWA WAZAZI WENYE WATOTO WALEMAVU DODOMA....
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Na Peter Mkwavila,Dodoma
WAZAZI wenye watoto walemavu mkoani Dodoma wamesema kuwa mpango wa utekelezaji wa elimu bure kwa shule ya misingi na sekondari kwa upande wao ni mzigo usiobebeka na hakuna faida kwao.

Wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti mjini hapa walisema kuwa mpango huo wa elimu ya bure haujawagusa watoto wenye ulemavu ukizingatia kuwa karibu mahitaji yao wanayotakiwa kuwa nayo yanashughulikiwa na wao wenyewe.

Athumani Bakari mkazi wa kijiji cha kigwe ambaye ana mtoto mwenye ulemavu wa viungo alisema ameshindwa kumwandikisha shule kutokana na kushindwa kumpatia baiskeli ya kumwezesha kumfikisha shuleni.

Alisema watoto hao wenye ulemavu wa aina mbalimbali wanatakiwa kuwa na vifaa kama vile baiskeli ya magudurudumu matatu,mashine ya kuandikia kwa watoto wasiona na wale malbino wanastahili kuwa na vitabu nyenye maandishi makubwa,
Halima Juma wa kijiji cha Buigiri alisema kuwa elimu bure iliyotangazwa bado ni changamoto kwao kutokana na serikali kushindwa kugharimikia kwa vifaa vinavyotumiwa na watoto hao wenye ulemavu kama walivyowajibika kununua kwa ajii ya shule ya misingi na sekondari.
Kwa upande wake Katibu wa Shirikisho la watu wenye ulemavu mkoa wa Dodoma Justus Ng’wantalima ameiomba serikali kuondoa gharama za vifaa vya watu wenye ulemavu kwa upande wa watoto ili waweze kunufaika na elimu hiyo ya bure.
Alisema kuwepo kwa gharama kubwa ya vifaa hivyo bado wazazi wenye watoto wenye ulemavu wataendelea kuwaficha majumbani na lundo la wasiojua kusoma na kuandika litazidi kuwepo wakiwemo na ombaomba wa mitaani pia.
Hata hivyo amewataka wazazi na walezi wenye watoto walemavu kuhakikisha wanawapeleka shule pamoja na changamoto watakazo kutananazo zikiwemo miundumbinu na ukosefu wa vifaa wanavyotakiwa kuwanavyo.
Mwisho

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / MPANGO WA ELIMU BURE BADO NI MZIGO KWA WAZAZI WENYE WATOTO WALEMAVU DODOMA....

No comments :