Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » SIMBA YAZINDUKIA UPYA KWA MTIBWA, MATOKEO MENGINE NI HAYA HAPA
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Wachezaji wa Simba Ibrahim Ajib (kushoto), Amis Kiiza (katikati) na Peter Mwalyanzi (kulia) wakishangilia goli lililofungwa na Amis Kiiza
Kocha wa Simba Mganda Jackson Mayanja ameanza vizuri kibarua chake baada ya kukiongoza kikosi cha ‘wekundu wa Msimbazi’ Simba kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye mechi yake ya  kwanza ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara akiwa kama kocha wa timu hiyo  ambayo siku chache zilizopita imemfukuza aliyekuwa kocha wake mkuu Dylan Kerr.
Goli la Simba limefungwa na Amis Kiiza katika dakika ya nane kipindi cha kwanza bao ambalo limedumu hadi dakika ya 90 ya mchezo na kuishuhudia Simba ikiondoka uwanjani na pointi tatu mbele ya Mtibwa.

Kikosi cha Simba kilikuwa chini ya kocha Jackson Mayanja aliyejiunga hivi karibuni kama kocha msaidizi wa timu hiyo kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa kocha msaidizi wa wekundu wa Msimbazi Selemani Matola ambaye alijiuzulu kutokana na kutoelewa na aliyekuwa kocha mkuu Dylan Kerr.
Baada ya kuondoka kwa Kerr Mayanja alipewa jukumu la kuinoa Simba akiwa kama kocha mkuu hadi hapo atakapopatikana kocha mkuu atakayechukua mikoba ya Kerr aliyetimuliwa baada kufungwa na Mtibwa Sugar kwenye michuano ya Mapinduzi Cup wiki iliyopita visiwani Zanzibar.
Mchezo huo ulikuwa ni kwanza kwa Mayanja na amefanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya timu iliyowatoa kwenye Mapinduzi Cup wakati huo Mayanja alikuwa jukwaani akishuhudia mtanange huo. Ushindi wa leo wa kikosi cha Simba ni sawa na kulipa kisasi kwa wakatamiwa hao.
Mtibwa Sugar walicheza soka safi licha ya kupoteza mchezo huo lakinin watajilaumu wenyewe kwa kupoteza nafasi walizozipata kwenye mchezo huo.
Matokeo ya michezo mingine iliyopigwa leo kwenye viwanja vingine ni kama ifuatavyo:
JKT Ruvu 1 – 5 Mgambo JKT 
Toto Africans 0-1 Tanzania Prisons 
Stand United 1-0 Kagera Sugar 
Mbeya City 1-0 Mwadui FC 
Coastal Union 1-1 Maji Maji FC

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / SIMBA YAZINDUKIA UPYA KWA MTIBWA, MATOKEO MENGINE NI HAYA HAPA

No comments :