Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » TAASISI GINCO YAENDESHA SEMINA KWA WANAWAKE WAJASIRIAMALI
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Gihon Needy Comfort Organization (GINCO), Rebecca Stanford (kushoto), akiwaonesha nguo wanawake wajasiriamali katika semina ya siku moja ya kuwaongezea uwezo na stadi za maisha iliyofanyika mwishoni mwa wiki Makao Makuu ya Taasisi hiyo Ukonga jijini Dar es Salaam.
Semina ikiendelea. 

WANAWAKE wametakiwa kuwa na moyo wa kuthubutu ili kujiletea maendeo badala ya kukaa bure bila kazi jambo litakalo waondoa katika maisha ya utegemezi.

Mwito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Gihon Needy Comfort Organization (GINCO), Rebecca Stanford wakati akizungumza na wanawake wajasiriamali katika semina ya siku moja ya kuwaongezea uwezo na stadi za maisha iliyofanyika Ukonga Dar es Salaam Jumamosi.

“Kuna fursa nyingi ndani ya ujasiriamali hivyo mnapaswa kuthubutu kwa kubuni vitu mbalimbali kama utengenezaji wa nguo, viatu, ufugaji, urembo na vingine vingi badala ya kusubiri kupewa” alisema Stanford.

Akizungumzia kuhusu taasisi hiyo, Stanford alisema wamejikita zaidi katika kushirikisha jamii, wahisani, wadau wa maendeleo ikiwemo Serikali kupigania ustawi wa kiuchumi, kijamii na kiutamaduni ili kuondoa umaskini, unyanyasa na uonevu kwa lengo la kuleta maendeleo endelevu.

Aliongeza kuwa Shirika hilo si la kisiasa, kidini wala kibiashara na limeundwa kwa nia ya kuhudumia na kusaidia jamii na limesajiliwa chini ya Sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali Namba 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2005 na kupata namba ya usajili 00NGO/08289.
 
About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / TAASISI GINCO YAENDESHA SEMINA KWA WANAWAKE WAJASIRIAMALI

No comments :