Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » BORA KUPATA MAENDELEO KWA KILA MTANZANIA TENA YA HAKI KWA KUWAUMIZA WALIO WACHACHE LAKINI SIO KUWANEEMESHA WACHACHE ISIVYO HAKI KWA KUWAUMIZA WALIO WENGI...
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

{Maoni Binafsi}

“watumbue tu kama inawezekana pia wapasue kabisaaa, ili tuipate Tanzania yetu na sio Tanzania ya wakoloni {ukoloni mamboleo}”

“Hivi ikiwa viongozi wakishindwa kusimamia nafasi zao Rais anafanya nini zaidi ya kujiuzulu? na ikiwa si kujiuzulu sio bora kuzifanya kazi yeye mwenyewe?”

“nchi hii ikiwa katika mahangaiko kwa wananchi wake kuishi chini ya dola moja wakati ambao tajiri mmoja mlo wake mmoja tu unafikia hadi zaidi ya shilingi elfu 50 hii ni kufuru”

Nashindwa kuwaelewa wanadamu hasa wanasiasa na wanaowafuata, maana wakati mtu akiharibu humuita dhaifu, mtuhumiwa, mwoga, mzito katika maamuzi, Mzigo n.k... lakini pia akiwa mwepesi kuchukua maamuzi huitwa mkurupukaji, mvunja katiba, asiyejua majukumu yake n.k.

Hivi ikiwa viongozi wakishindwa kusimamia nafasi zao Rais anafanya nini zaidi ya kujiuzulu? na ikiwa si kujiuzulu sio bora kuzifanya kazi yeye kwa kuwasimamisha wapotovu na kuwachagua wanaoweza kuendana na kinachotakiwa na watanzania walio na uchungu na nchi yao? sasa mi nashangaa siku hizi kuna watu waliojiita wanamapinduzi, wanaharakati na pengine tungewaita wanamabadiliko tunawashuhudia wakibadilika na kuwa wana haki za kibinadamu kwa kuwatetea wakosaji kisa wanataka kuonesha Rais ana mapungufu katika hatua zake anazozichukua.

Mi nadhani kwa mtazamo wangu, kwa kiwango zaidi ya changu cha kufikiri,na upeo wa wenye akili na uelewa wa kuchanganua mambo ni bora kupata maendeleo kwa kila mtanzania tena ya haki kwa kuwaumiza walio wachache lakini sio kuwaneemesha wachache isivyo haki kwa kuwaumiza walio wengi...

Ni bora Rais JPM akakubali maneno yasiyo yenye weledi kutoka kwa wasioona kinachotakiwa kwa wakati huu, ayasikilize lakini katika utendaji aendelee na mipango yake yenye kuitafuta Tanzania yenye NEEMA kwa watanzania wote.

Na kutoa fedha kwenye wizara moja na kupeleka kwenye wizara nyingine wapo wanaodai sio kazi ya rais, sasa swali ni kwamba mbona kikiharibika kitu analaumiwa rais? na ni nani mwenye kazi hiyo ikiwa wenye kazi hiyo katika awamu zilizopita walishindwa kufanya kazi yao na kusababisha athari zilizokuwa mtaji kwa wapinzani kuiangusha serikali.

Mi nadhani umefika wakati wa wapinzani wa serikali kukubaliana na serikali kufanya kazi moja ambayo ni kuwasaidia wananchi kwa kuisaidia serikali kufikia malengo chanya ambayo ndio sababu kubwa ya kuwepo kwa upinzani licha ya kwamba natambua hakuna uwezekano wa kukubaliana na hili kwa asilimia mia moja lakini tunaweza kujaribu tukiweza tuipitishe na tukishindwa tukubali tumeshindwa na kuangalia mengineyo.

Kuna mambo mengi ambayo rais amelalamikiwa ikiwa ni pamoja na {utumbuaji wa jipu} kusimamishwa kazi  Meya wa jiji la Dar es salaam Wilson Kabwe wakidai kavunja haki za binadamu kwa kumtumbua hadharani...Khaaa!! ulitaka iwe siri wakati kila kitu kinajulikana kilichokuwa kikitokea nah ii ni kwa mujibu wa hotuba ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaa katika siku ya Uzinduzi wa daraja la Mwalimu Nyerere mwezi huu.

Nachoweza kusema sasa ni kwamba alikosekana tu mtu wa kumtumbua,, lakini wengine wanaona kuwa hata huyu aliyejitoa mhanga kwa ajili ya watanzania bado wanamuona hana maana na anatakiwa kufuata sheria, sheria ipi inayokiukwa lakini wakati huo huo ilivunjwa na wengine nasi kupiga kelele kumhitaji mtu sahihi wa kulishughulikia?

Umefika sasa wakati wa kila mtu kusimamia kitengo chake wakati huo huo akishindwa basi bosi wake akifanye kwa kuwajibika au kuwajibishwa nah ii sasa ndio itajenga heshima zaidi katika taifa tajiri kwa mali lakini maskini kwa matumizi.

Leo ni aibu kwa uongozi kutokana na uhuru waliopatiwa wananchi na wanasiasa wakiwemo viongozi kutokana na usaliti wanaofanya kwa wananchi kwa kutotimiza ahadi zao kwa wananchi lakini muda huo huo wakishutumiwa kumiliki mali za watanzania kinyume cha sheria huku nchi hii ikiwa katika mahangaiko kwa wananchi wake kuishi chini ya dola moja wakati ambao tajiri mmoja mlo wake mmoja tu unafikia hadi zaidi ya shilingi elfu 50 hii ni kufuru na matusi kwa watanzania wa kipato cha chini.

Huu sasa ni muda wa Rais JPM kuhakikisha mazoea na dharau za viongozi anaviondoa ikiwezekana kwa kuvunja katiba ya nchi maana itafikia hata mahakimu na majaji wanahitajika kutumbuliwa sasa hapa pasipokutumia katiba isiyo rasmi atashindwa kwa hiyo ni lazima kupindisha sheria ili kuokoa kinachotaka kupotea au kilichopotea tayari….

Rais John Pombe Joseph Magufuli, ni ombi langu kama inawezekana lipitishe, kama ukiona haliwezekani tafadhali ni bora ulazimishe wanyonge wa mali tajiri wa mawazo wako nyuma yako kukusaidia kuwamaliza wote walio kinyume na kasi yako, watumbue tu kama inawezekana pia wapasue kabisaaa, ili tuipate Tanzania yetu na sio Tanzania ya wakoloni {ukoloni mamboleo}

Wakati mwingine amekuwa akilazimishwa kutenda kinyume cha sheria kwa sababu mambo hayo yanaonekana kuwawia vigumu kukamilisha adhima yao, mfano ni mgogoro wa kisiasa Zanzibar, Rais JPM alipolazimishwa kutoa maamuzi juu ya vurugu zile angali wakijua kabisa hana mamlaka hiyo kisheria na imeandikwa katika sheria ya nchi hii kwa mujibu wa Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Damian Lubuva lakini pi aMh. Mwenyewe aliwahi kugusia suala hilo baada ya kubanwa akaamua kulitolea ufafanuzi.

Hitimisho: ifike wakati kila mtu afanye kazi yake, lakini akishindwa siyo lazima aseme lakini msimamizi wake amwajibishe na akishindwa pia nae awajibishwe na wananchi wenyewe, lakini sio sawa kumtuhumu rais kwa mapambano aliyonayo maana kesho pia tutakuja kulalamika juu ya unyanyasaji,wizi na matukio mengineyo dhidi ya viongozi wetu wasio waadilifu kwa umma.

“Asante kwa kupat anafasi katika ukurasa huu kuelezea haya”.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / BORA KUPATA MAENDELEO KWA KILA MTANZANIA TENA YA HAKI KWA KUWAUMIZA WALIO WACHACHE LAKINI SIO KUWANEEMESHA WACHACHE ISIVYO HAKI KWA KUWAUMIZA WALIO WENGI...

No comments :