Mabingwa watetezi wa taji la Ligi ya Vodacom Tanzania, Yanga Jumapili watashuka dimba la taifa Dar es Salaam, kuikabili Kagera Sugar ukiwa ni mchezo wa kiporo mzunguko wa 22
Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu na wenye ushindani mkali kwani wageni Kagera wanapambana kuepuka kushuka daraja kutokana na nafasi mbaya waliyopo nafasi ya 11 na pointi 25, wakati Yanga yenye pointi 50 inapigana kurudi kwenye nafasi ya kwanza kwa kuiengua Simba iliyopo kileleni na pointi zake 57 lakini ikiwa mbele ya michezo.
Katika mchezo wa mwisho timu hizo zilipo kutana kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi Taboro, Yanga ilichomoza na ushindi wa mabao 2-0, hivyo hiyo ni nafasi pekee kwa Kagera kuweza kusawazisha.
Katika mchezo wa kesho Yanga huenda ikatumia kikosi chake kamili baada ya katikati ya wiki kwenye mchezo wa kombe la FA, dhidi ya Ndanda FC, kuwakosa nyota wawili wakimataifa Haruna Niyonzima na Amissi Tambwe.
Kocha Hans van der Pluijm, amesema wanaupa umuhimu mkubwa mchezo wa kesho na kilicho cha msingi kwao ni pointi tatu ambazo zitafufua matumaini yao ya kurudi kileleni.
Pluijm amesema atatumia kikosi chake kamili kwakua anaijua Kagera ni timu nziri iliyoanza kuimarika licha ya kuanza vibaya msimu huu na mbali na kutaka ushindi lakini anataka kushinda mabao mengi ambayo anaamini yatawabeba siku zijazo.
“Nimchezo mgumu kwasababu tunacheza kwa presha katika mechi hizi za viporo na lengo letu ni kurudi kwenye nafasi yetu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda mechi zetu zote na kurudi kwenye uongozi wa ligi,”amesema Pluijm.
Kwaupande wake kocha wa Kagera Sugar, Adolfu Rishard, amesema wanafahamu kuwa kesho wanakutana na timu ngumu na bora Tanzania Yanga, lakini hawawaogopi na wamejianda kupambana nao na kupata ushindi.
Rishald amesema anajivunia kuimarika kwa kikosi chake katika mechi za hivi karibuni hivyo anatarajia kikosi chake kuonyesha kandanda safi na kulipa kisasi cha mabao 2-0, walichofungwa kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza.
Kocha huyo amesema amekuja Dar es Salaam na jeshi lake lote akiwemo winga machachari Paul Ngwai, kiungo Daud Jumanne na nahodha wake George Kavilla, akiamini uzoefu wao watawazuia Yanga kutamba wakiwa nyumbani.
“Bado tupo katika sehemu mbaya ya hatari endapo tutapoteza mchezo wa kesho na mingine inayokuja tutajiweka katika wakati mgumu hivyo nilazima tuanze kufufa matumaini kuanzia mchezo huu wa kesho,”amesema Rishard
Endapo Yanga itashinda itafikisha pointi 53 na kubakiwa na alama nne huku ikiwa na michezo mitatu ili kuifikia Simba.
No comments
Post a Comment