Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » IDADI YA WADAIWA 21,721 WAPYA WAMEJITOKEZA BODI YA MIKOPO, ZAIDI UNAWEZA KUJIPAKULIA HAPA
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) March 14 2016 ilitoa  agizo la siku 60 kuwa wadaiwa wa mikopo ya elimu  ya juu kujitokeza ili kuanza kulipa madeni yao, wadaiwa wapya 21,721 wamejitokeza ili kuanza kulipa madeni yao.
Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)  Robert Kibona  amezungumza na waandishi wa habari May 20 2016 na kutoa tahtmini kuhusu agizo lililotolewa na bodi hiyo kwa wanufaika wa mikopo na waajiri ili kutimiza wajibu wao kisheria.
Kibona alifafanua kuwa jumla ya Shilingi bilioni 151.5 zinatarajiwa kurejeshwa na wadaiwa hao ambao walikopeshwa ili kuwawezesha kupata elimu yao ya juu katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi kuanzia mwaka 1994.
>>>“Lengo la agizo lilikuwa ni kuhahakisha madeni yote yaliyoiva yanakusanywa ili kuongeza uwezo wa kukopesha watanzania wengi zaidi na agizo hili limeisha Mei 13 mwaka huu.” Kibona
Kwa mujibu wa Kibona, kati ya wadaiwa waliopatikana, wadaiwa 19,528 walipatikana baada ya Bodi kuchambua taarifa za waajiriwa zilizowasilishwa na waajiiri na wadaiwa wengine wapatao 2,007 walijitokeza kwa hiari.
Waajiri wana wajibu wa kisheria wa kuwasilisha taarifa za waajiriwa wao, baadhi yao walifanya hivyo katika siku hizo sitini na tukawabaini wadaiwa hao, tunawapongeza waajiri kwa ushirikiano walioutoa na wanufaika wote waliojitokeza kwa hiari”  Kibona.
Bodi imeongeza siku 30 za ziada kuanzia May 20, 2016 kwa wadaiwa waliobaki kujitokeza na uamuzi huo umetokana na tathmini iliyoonyesha kuwa kuna idadi kubwa ya waajiri na wanufaika wanaoendelea kujitokeza.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo Bw. Cosmas Mwaisobwa alisema kuwa kiwango cha ukusanyaji wa madeni kwa mwezi kinatarajiwa kuongezeka kutoka shilingi bilioni 2.7 zinazokusanywa hivi sasa na kufikia shilingi bilioni 8 ifikapo mwezi Juni 2016.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / IDADI YA WADAIWA 21,721 WAPYA WAMEJITOKEZA BODI YA MIKOPO, ZAIDI UNAWEZA KUJIPAKULIA HAPA

No comments :