Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » KISPOTI CHACHE ZILIZOJITOKEZA HADI SASA
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

YANGA SC

Kikosi cha Yanga kimerejea nchini baada ya kupoteza mechi yake ya tatu ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Medeama nchini Ghana.

Yanga wametua nchini kwa mafungu, wakianza na kundi la kwanza lililotua jijini Dar es Salaam saa 8 usiku.

Baadaye saa 2 asubuhi, kundi la pili likiongozwa na kocha Hans van der Pluijm nalo likawasili.

Ingawa mashabiki wamekuwa wakijaribu kujipa moyo, lakini hali halisi hasa ni kwamba Yanga haina nafasi tena ya kufuzu hatua ya nusu fainali.

Kocha Pluijm, amesisitiza makosa ambayo waliyazungumza, yamefanyika na kuwafanya wapoteze mchezo.

Ingawa alilalamika suala la safari ndefu hasa ile ya basi baada ya kuwa wamewasili Ghana.

SIMBA SC

Viongozi na wanachama mbalimbali wa Simba watachangia damu katika hospitali mbalimbali.

Rais wa Simba, Evans Aveva amesema watafanya hivyo ikiwe ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya Simba kwenda kusherekea miaka 80 ya klabu hiyo.

Siku kamili ya sherehe itakuwa ni Agosti 8 wakati tamasha la Simba Day litakapofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijiji Dar es Salaam.

Kocha Zdravko Logarusic anarejea jijini Dar es Salaam, safari hii akiwa amepewa kazi ya kukipima kikosi cha Simba.

Logarusic maarufu kama Loga, anakuja nchini ndani ya siku chache akiwa ameongozana na kikosi chake cha Inter Club cha Angola.

Kikosi hicho kitapambana na Simba katika mechi ya Simba Day ambayo itapigwa Agosti 8, siku ambayo Simba itauwa inatimiza miaka 80.

Tayari Logarusic alikuwa amesema angetamani kukutana na Simba na kuwaonyesha kazi yake ilivyo bora.

Sasa Simba inanolewa na Kocha Joseph Omog raia wa Cameroon na imejichimbia mjini Morogoro.

Chini ya kocha huyo, Simba imecheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya Polisi Morogoro iliyo daraja la kwanza na kuivurumisha kwa mabao 6-0.

AZAM FC

Mshambuliaji raia wa Zimbabwe, Brian Abbas Amidu ametua nchini tayari kujaribiwa katika kikosi cha Azam FC.

Amidu amesafirishwa hadi mjini Zanzibar ambako Yanga imeweka kambi yake kujiandaa na Ligi kuu Bara msimu mpya wa 2016-17.

Azam FC inahaha kupata straika kwa kuwa mshambuliaji wake Kipre Tchetche amegoma kurejea nchini.

KIMATAIFA

TP MAZEMBE
Wakati Yanga ya Tanzania imepoteza matumaini kabisa ya kusonga mbele hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho, TP Mazembe, leo wamejihakikishia nafasi hiyo.

TP Mazembe imeilaza Mo Bejaia kwa bao 1-0 katika mechi iliyopigwa mjini Lubumbashi, mfungaji akiwa Rainford Kalaba katika dakika ya 61.

Kwa ushindi huo, Mazembe imefikisha pointi 10 ambazo zinaipa uhakika kubaki katika nafasi ya kwanza au ya pili kulingana na matokeo ya mechi mbili zilizobaki kwa kila timu ya Kundi A.

Bejaia wana mechi mbili, dhidi ya Yanga ugenini na Medeama nyumbani wakati TP Mazembe mbili zao, moja ni ugenini dhidi ya Medeama na nyumbani dhidi ya Yanga.

Kama itashinda mechi nyingine moja kati ya hizo mbili, TP Mazembe itakuwa imejihakikisha kukaa kileleni mwa kundi hilo.

Kwa muonekano, Mo Bejaia iliyo katika nafasi ya pili na Medeama nafasi ya tatu, kila moja ina nafasi kwa kuwa kila moja ina pointi tano.

Lakini uwezekano wa kufuzu unabaki kwa moja kwa kuwa zitakutaka. Kama zitatoka sare, zitakuwa zimeipa nafasi Mazembe kubaki kileleni lakini moja ikishinda, itakuwa imepata nafasi na moja kupoteza.

Bejaia watataka kushinda mechi dhidi ya Yanga jijini Dar es Salaam, ili mechi ya mwisho dhidi ya Medeama iwe fainali. Lakini Medeama nayo italazimika kuilaza Mazembe ugenini ili iwe isubiri mechi ya mwisho.

Kwa kifupi, sasa ushindani wa nafasi moja umebaki kwa Bejaia na Medeama huku Yanga ikiwa imeaga rasmi.

ASENAL WENGER
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger kuna uwezekano wa kukiacha kiti chake hicho cha umeneja kwa kocha wa kikosi cha Bournemouth Eddie Howe, hii ni kwa mujibu wa gazeti la Daily Star.
Taarifa zinadai kuwa Arsenal itakuwa sawa na mashabiki wengi watafurahi kumuona wenger akichomoka katika kikosi hicho baada ya majira ya joto kikosi hicho kilipoanza kumtafuta kocha mpya atakayemrithi mfaransa huyo aliyeingia katika kipindi cha miezi kumi na mbili ya mwisho ya mkataba wake.

ROGERS CUP
Mcheza Tenisi nambari moja kwa Uingereza Johanna Konta ameifikia hatua ya tatu ya Rogers Cup kwa kumchapa Mmarekani Vania King.
Mwana dada huyo amefikia hatua hiyo kwa ushindi wa 7-5 6-1 dhidi ya King.
Johanna Konta ambaye katika uchezaji Duniani yuko kwenye nafasi ya 14, katika hatua inayofuata atakutana na Mmarekani Varvara Lepchenko

BALOTELI
hatimae Klabu ya Hull City ya Uingereza imemsajili Mario Balotelli kutoka Liverpool kwa pauni milioni 26.
Hii imekuwa taarifa njema kwake kwani Liverpool haikuwa imempanga kucheza msimu huu.

Hata hivyo wachezaji mahiri wa soka kama kama vile Adrea Pirlo Wamesikitishwa na kushangazwa na kudorora kwa soka la Balotelli.

CARLOS TEVEZ
Star wa Boca Juniors star na straika wa zamani wa Manchester city,Manchester united  na Juventus Carlos Tevez amefichua kwamba alipigiwa simu na kocha wa chelsea Antonio Conte akimpa ofa ya kuichezea klabu ya Chelsea. 
Mshambuliaji huyo wazamani wa Juventus alikuwa akitarajia kutwaa kombe la pili la Copa Libertadores akiwa na Boca lakini timu yake iliishia nusu fainali baada ya kupoteza mbele ya klabu ya Independiente del Valle. 
Tevez amethibitisha kwamba Conte,ambaye ni kocha wake wa zaman akiwa juventus alimpa ofa hiyo iliyolenga kumrejesha Ulaya kwa mara nyingine lakini alikumbuka kwamba tayari alishastaafu soka la kimataifa na kuamua kuendelea kuchezea nyumbani kwao Argentina.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32-akizungumza na Radio La Red ya huko kwao anasema kuwa alikuwa akiendesha gari akiwa na familia yake, ambapo konte alimpigia simu na kumwambia kuwa alikuwa akiitaji forward na kumuuliza iwapo anaweza kucheza Chelsea.

Chelsea 1 - 0 Liverpool
Mfungaji- Gary Cahill  10'
1 - 0
 70' Cesc Fabregas-straight red card  

 AC Milan ft Bayern Munchen 5-3 penalties after 3-3 =90’

PSG FT Real Madrid 3-1

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / KISPOTI CHACHE ZILIZOJITOKEZA HADI SASA

No comments :