Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » AUAWA KWA TUHUMA ZA KICHAWI MKOANI RUKWA
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Mwanamke aitwaye Noelia Pintilila (80) Mkazi wa Kijiji cha Kanyezi Tarafa ya Mwazye, Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa ameuwawa kwa kupigwa kichwani na fimbo baada ya kutuhumiwa kuwa ni mchawi. 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Geoge Kyando aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa tano asubuhi kijijini hapo . 

Alisema siku hiyo ya tukio marehemu alikuwa nyumbani kwake akiwa anaendelea na shughuli ndogo ndogo za kila siku mara baada ya kuwa amemaliza kunywa chai ya asubuhi.

Kamanda Kyando alieleza wakati marehemu akiwa anaendelea na shughuli zake alifika mtuhumiwa wa mauaji hayo ambae jina lake limehifadhiwa alikuwa ni mgonjwa wa kifafa na ndipo alipomshuku marehemu kuwa ni mchawi amemroga ugonjwa wa kifafa. 

Hata hivyo marehemu alimkatalia kuwa yeye si mchawi na wala tabia hiyo ya ushirikina tangu kuzaliwa hajawahi kuwa nayo. 

Licha ya kujitetea huko mtuhumiwa huyo aliendelea kumshutumu kikongwe huyo kuwa yeye ni mchawi na ndiye aliyemroga ugonjwa wa kifafa. 

Baada ya mabishano hayo kuendelea kwa muda mrefu ndipo mtuhumiwa alipoanza kumpiga kwa fimbo kichwani marehemu Noelia hadi kufariki dunia hapo hapo .

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / AUAWA KWA TUHUMA ZA KICHAWI MKOANI RUKWA

No comments :