Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » MOTO WATEKETEZA NYUMBA 50 WAMILIKI WAKE WAKILA KRISMASI
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

MOTO mkubwa umezuka na kuteketeza nyumba zaidi ya 50 katika kisiwa cha Kasalazi kilichopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa mkoani Mwanza.

Tukio hilo lilitokea juzi saa 3:00 usiku, linadaiwa kuwa ni la nne kutokea kisiwani humo katika miaka ya karibuni.

Imeelezwa kuwa moto huo ulizuka na kuteketeza nyumba hizo huku wamiliki wake wakiwa kwenye shamra shamra za Krismasi.

Nyumba zilizoteketea kwa moto ni zile zilizojengwa kwa kutumia mabanzi ya miti, mbao na kuezekwa kwa maturubai, nyasi na baadhi kwa bati.Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kasalazi, Andrew Mkama, amesema  kuwa wakati tukio hilo linatokea, wakazi wengi wa kisiwa hicho walikuwa kwenye kumbi mbalimbali za starehe kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo zaidi ya miaka 2,000 iliyopita.

Mkama alisema alilazimika kupuliza filimbi kuashiria hatari na wananchi walijitokeza na kuanza jitihada za kuuzima moto huo licha ya kwamba tayari ulikuwa umeshasababisha madhara makubwa kwa kuunguza mali zote zilizokuwa ndani yake.
 
Hata hivyo alisema hakuna mtu aliyekufa wala kujeruhiwa kutokana na janga hilo.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, walisema moto huo umesababisha hasara kubwa kwao.

Mmoja wa mashuhuda hao, Raphael Bituro, anayemiliki duka la vinywaji, alisema baada ya kupulizwa filimbi kuashiria hali ya hatari, baadhi ya wateja wake walikurupuka bila kulipia vinywaji vyao na hivyo kusababisha apate hasara.

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole, alithibitisha kisiwa hicho kuungua kwa moto.

Kipole alisema ameagiza kufanyika kwa uchunguzi ili kubaini ukubwa wa madhara hayo na kuahidi kutoa taarifa zaidi atakapopewa ripoti hiyo.

Kisiwa hicho kinakadiriwa kuwa na wakazi zaidi ya 2,400 ambao hujihusisha na shughuli za uvuvi na ni miongoni mwa visiwa vinane vilivyopo kwenye Kata ya Bulyaheke wilayani Sengerema.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / MOTO WATEKETEZA NYUMBA 50 WAMILIKI WAKE WAKILA KRISMASI

No comments :