Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » MRADI MKUBWA WA UMEME WA BACKBONE UMEKAMILIKA, UTAZINDUALIWA JANUARI MWAKANI
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

MRADI wa umeme wa Backbone wa ujenzi wa njia kuu ya umeme ya msongo wa Kilovolti 400 ya urefu wa Kilomita 670 kutoka Iringa hadi Shinyanga kupitia mikoa ya Dodoma na Singida, umekamilika kwa asilimia 100, Meneja wa Mradi huo, Mhandisi  Khalid Reuben James amewaambia wahariri wa vyombo vya habari mjini Iringa leo Desemba 19, 2016.
 
Pia  mradi huo unaohusisha kukamilika kwa upanuzi wa vituo vine vya kupoza na kusambaza umeme kwenye mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida na Shinyanga utawezesha kuvipatia umeme vijiji takriban 121, vinavyopitiwa na mradi huo, alisema Mhandisi James.
 
“Mradi huu ni wa muhimu sana kwenye gridi ya taifa kwa sababu utaongeza uwezo wa kusafirisha umeme kutoka kanda ya Kusini Magharibi, ambako kuna vyanzo vingi vya umeme na kupeleka Kanda ya Kaskazini Magharibi ambako kuna shughuli nyingi za kiuchumi ikiwemo migodi ya madini.” Alifafanua Mhandisi James.
 
Kwa mujibu wa Mhandisi huyo, mradi huo ulianza mwaka 2013, na ulikadiriwa kugharimu kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 470, ambazo zimetolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na wafadhili wakiwemo, Benki ya Dunia, dola za Kimarekani, milioni 150, Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB),  na Shirika la Maendeleo la Kijapani, (JICA), Dola za Kimarekani milioni 129.7, Benki ya Uwekezaji ya nchi za Jumuiya ya Ulaya, (EIB), Dola za Kimarekani milioni, 134.5, Shirika la Kiuchumi la Maendeleo ya Korea ya Kusini, (EDCF), Dola za Kimarekani milioni 36.416, na Serikali ya Norway, Sweden na Tanzania, kupitia kwa wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dola za Kimarekani milioni 33.4.
 
“ Ndugu zangu, mradi huu unatoa hakikisho kwa serikali kuwa mipango yake ya kujenga uchumi wa viwanda unawekana pasina shaka, kwani mradi huo mkubwa, utawezesha sasa, kuwapatia wateja umeme ulio bora na wa uhakika,” alsiema.
 
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini, wako kwenye ziara ya kutembelea mradi huo ambao unatarajiwa kuzinduliwa rasmi mapema mwezi Januari, 2017.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / MRADI MKUBWA WA UMEME WA BACKBONE UMEKAMILIKA, UTAZINDUALIWA JANUARI MWAKANI

No comments :