Takwimu zinaonesha China inashika nafasi ya kwanza kwa kuwa na Idadi kubwa ya watu Duniani ambapo ina jumla ya watu Bilioni 1.38, nafasi ya pili ni India ambayo ina jumla ya watu Bilioni 1.31, hao sio watu wachache mtu wangu kwa sababu ukiangalia Dunia nzima ina jumla ya watu Bilioni 7 !!
Tatizo la ukosefu wa ajira ni tatizo kubwa sana sasahivi kila sehemu Duniani, nchi ya India inaingia kwenye stori kubwa kwa leo… ishu ni kwamba Serikali ya India ilitangaza nafasi 368 za kazi kwa Walinzi pamoja na Wahudumu wa Chai Maofisini, lakini unaambiwa kwenye nafasi hizohizo 368 watu waliojitokeza kuomba nafasi walikuwa watu Milioni 2.3.
Maofisa wa Serikali wamesema kama kila mtu aliyetuma maombi ya kazi akiitwa kwenye Interview maana yake ni kwamba itachukua miaka minne mpaka kuwapata watu watakaoajiriwa kwenye nafasi hizo.
Wengi walioomba kazi wanasema walipoona tangazo ilibidi watume maombi kwa sababu hakuna ajira na maisha ni magumu.
Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa, UN zinaonesha mpaka kufikia mwaka 2030India itaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu, ikifuatiwa na China na Marekani.
No comments
Post a Comment