Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker akiwa na Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan |
Viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya leo watakutana katika
mkutano wa kilele, kujaribu kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa wahamiaji
barani Ulaya pamoja na kuishawishi Uturuki kuwapa hifadhi wahamiaji
wanaotokea Syria
Mkutano huo wa kilele unalenga kufanya kazi pamoja na nchi zilizo nje ya
mipaka ya bara la Ulaya ili bara hilo liweze kupambana na mgogoro
mkubwa wa wahamiaji kuwahi kutokea tangu vita vya pili vya dunia.
Jambo muhimu litakalozingatiwa katika mkutano huo wa leo ni kuishawishi Uturuki kuukubali mpango wa Umoja wa ulaya, unaoitaka nchi hiyo kuwapa hifadhi wahamiaji milioni mbili, huku Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akiwa anelekea nchini humo Jumapili kwa ajili ya mazungumzo.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akiwa katika bunge la Ujerumani - Bundestag |
Merkel ameongeza kwamba lazima kuwepo mshikamano barani Ulaya juu ya mgogoro wa wahamiaji
Wakati huo huo, Makamu wa Rais wa Umoja wa Ulaya Frans Timmermans pamoja na maafisa waandamizi wingineo, wamewasili Uturuki jana kuishinikiza serikali ya nchi hiyo kukubali mpango huo wa Umoja wa Ulaya, baada ya kuahirisha safari hiyo kutokana na shambulio la mabomu la mjini Ankara mwishoni mwa juma lilopita.
No comments
Post a Comment