Jana kocha Juma Mwambusi alianza
rasmi kibarua chake kwenye kikosi cha Yanga wakati mabingwa hao watetezi
wakijiandaa na mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya mabingwa wa
Kagame Cup timu ya Azam FC mchezo unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi hii
kwenye uwanja wa taifa.
Mwambusi amesema anashukuru kwa
mapokezi mazuri ndani ya kikosi cha Yanga lakini akaomba apewe muda na
ushirikiano na wanajangwani huku akiitanguliza Yanga mbele halafu
wachezaji na mashabiki baadae.
“Namshukuru Mungu nimepokewa
vizuri nadhani nitatoa ushirikiano wa kuweza kufanya kazi vizuri.
Mwalimu Hans amefurahi kwasababu alikuwa anataka mtu mchapakazi na
anasema siku nyingi amekuwa ananifatilia kwahiyo anafurahi kufanya kazi
na mchapakazi kama yeye alivyokuwa anataraji”, amesema Mwambusi ambaye
kwa sasa ndiye kocha msaidizi wa Yanga.
“Mimi nataka nijifunze mengi
kabla sijaingia sana mtamboni, mechi ya Jumamosi tunacheza na Azam
ambayo tunaijua kwasababu tumeshacheza nao kwahiyo ni kupeana mawazo
nini cha kufanya kwenye mechi hiyo ya Jumamosi”.
“Nimekutana na wachezaji wangu
niliowahi kuwafundisha Moro United, Mbeya City na wengine tukiwa
tumekutana kwenye mechi lakini mambo yanakwenda vizuri na wao wamefurahi
na kuonekana wanaungana na mwalimu ambaye walikuwa nae siku za awali”.
“Kikubwa naomba nipate uhirikiano
kutoka kwa wana-Yanga tushikamane, tupeane muda ili tuweze kufanya kitu
kizuri, Yanga kwanza halafu wachezaji na mashabiki baadae”.
No comments
Post a Comment