Mkuu wa mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa akizungumza na viongozi wa dini mkoa wa dodoma |
Dr Brown Mwakiipesile askofu mkuu |
Kaimu Sheikh Mkuu mkoani dodoma Ahmed Said |
Katika maombi ya ufunguzi wa mkutano wa viongozi wa dini |
mchungaji Maliga wa kanisa la TAG nkhuhungu mkoani dodoma |
RPC mkoani dodoma David misime akitoa onyo kwa watanzania kupitia viongozi wa dini |
RPC mkoani dodoma David misime akitoa onyo kwa watanzania kupitia viongozi wa dini |
Kaimu Sheikh mkuu mkoa wa dodoma Ahmed Said |
Na mwandishi wetu
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Luteni mstaafu Chiku gallawa amewataka
viongozi wa dini kuendelea kuhubiri amani kwa waumini wao ili kuhakikisha
uchaguzi unaotarajiwa kufanyika oktoba 25 mwaka huu yaani siku nne zijazo.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa mkutano
na viongozi wa dini mkoani hapa waliokusanyika katika ukumbi wa Tresury Square
kwa lengo la kuzungumza juu ya suala la amani mkoani hapa kabla, wakati na baad
aya uchaguzi.
Mkuu huyo pia ametanabaisha kuwa
kuna baadhi ya viongozi waliounda vikundi vya vijana kwa lengo la kufanya fujo
kwa kuhofia kuwa tayari wameshashindwa na hivyo kujikita kuwapotosha vijana ili
kufanya vurugu siku ya uchaguzi.
Mkuu huyo wa mkoa ameongeza kuwa serikali inayo
mamlaka ya kutangaza juu ya wajibu wa wapiga kura baada ya kupiga kura,kutokana
na agizo alilolitoa Rais Jakaya Kikwete la wapiga kura kuondoka katika vituo
vya kupigia kura.
Akikazia kuhusu suala hilo Kamanda mkuu wa polis
mkoa wa Dodoma David Misime amesema kutoakana na mamlaka ya kisheria tume ya
uchaguzi inayo mamlaka ya kuwapa utaratibu mpya ili mradi kulinda amani.
RPC kaongeza kuwa wazazi
wanao wajibu wa kuwakalisha chini vijana wao juu ya kujiepusha na
makundi ya siasa kwani wamekuwa wakitumika sana hasa walio na umri chini
ya miaka 17.
Baadhi ya viongozi wa
dini nao wamezungumzia kuhusu
upotovu wa maadili kwa vijana wa kisasa pamoja na kuwaonya viongozi wa
dini
kujihusisha na masuala ya kisiasa kwani kwa kufanya hivyo kutasababisha
mgawanyiko miongoni mwa waumini wao na kuleta malumbano yasiyo na tija
kwao na taifa kwa ujumla.
Fungua hapa kusikiliza kauli ya RPC na RC dodoma juu ya mita 200 za Tume
No comments
Post a Comment