Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeanza kikao chake leo kwa wabunge wateule kumpitisha Mh Job Ndugai kuwa spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa miaka mitano ya uongozi mpya.
Wakati akijinadi mbele ya wabunge wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mkoani hapa,amedai kuwa kikubwa atakachohitaji kukizingatia ni kuhusu suala la ushirikiano, haki na usawa miongoni ya wabunge pasipo kujali itikadi zao za kivyama.
Katika hatua hiyo iliyoanza majira ya asubuhi leo ilianza kwa kupiga
kura kisha kumpitisha mh Job Ndugai kupitia CCM Kuwa spika mpya na
hatimaye kuanza zoezi zima la kuwaapisha wabunge waliochaguliwa na
wananchi na wale waliopitishwa viti maalum.
Wagombea wanane waliwania kiti cha spika akiwemo aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge la kumi ambaye ni mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM na mpinzani wake mkubwa anatarajia kuwa mgombea wa Chadema Bwana Goodluck Ole Medei.
Wengine ni waliokuwa wanawania kiti hicho ni pamoja na Peter Sarungi (AFP),Hassan Kisabiya (N.R.A),Dkt Godfrey Malisa (CCK),Job Ndugai (CCM),Goodluck Ole Medeye (CHADEMA), Richard Lymo (T.L.P),Hashimu Rungwe (CHAUMA) na Robert Kisinini kutoka DP.
DENICE

No comments
Post a Comment