Kenya inaendeleza harakati kali za kidiplomasia kujaribu
kuzishawishi nchi wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC)
kuizuia korti hiyo ya kimataifa kuendelea na kesi dhidi ya raia wake
wawili akiwemo Naibu Rais, William Ruto.
Nchi zilizosaini mkataba wa Roma uliopelekea kuanzishwa ICC zinatarajiwa kukutana wiki hii kutathmini utendaji wa mahakama hiyo. Kenya imekuwa ikizishawishi nchi za Afrika kuunga mkono mabadiliko ya sheria na kanuni za uendeshwaji wa korti hiyo ili kuathiri mwenendo wa kesi zinazomkabili Naibu Rais wa nchi hiyo William Ruto na mwanahabari Joshua arap Sang.
Viongozi wakuu wa ICC akiwemo mwendesha mashtaka, Fatou Bensouda wametoa wito kwa nchi wanachama kutochukua hatua zozote zitakazohujumu uhuru wa korti hiyo. Kwenye taarifa yao, viongozi wa ICC wamesema kuhujumu uhuru wa mahakama hiyo kutapelekea kushitadi mwenendo wa kupuuzwa sheria za kimataifa.
Naibu Rais wa Kenya, William Ruto na mwanahabari, Joshua Sang wanakabiliwa na mashtaka ya kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo zaidi ya watu 1400 walipoteza maisha.

No comments
Post a Comment