Viongozi wa mkutano
wa G20 nchini Uturuki wamesema wanamipango ya kuweka nguvu zaidi
kupambana na vitendo vya kigaidi hasa kwa kuvunja mianya ya ufadhili wa
kifedha kwa makundi ya kigaidi, Rais wa Urusi Vladmir Putin amesema njia
hiyo inapewa kipaumbele.
Nae Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema kuwa mashambulizi ya Paris yalikuwa yakipangwa nchini Syria lakini yaliandaliwa nchini Ubelgiji.Wapelelezi wanashuku kuwa mtu aliyekuwa anasuka mipango hiyo ni Abdelhamid Abaaoud, mwenye miaka 27, mbelgiji mwenye asili ya morocco, anatoka katika wilaya ya Molenbeek.
Polisi nchini Ubelgiji wamewashutumu watuhumiwa wawili na wanamtafuta Salah Abdeslam, raia wa ufaransa aishie mjini Brussels ambaye nduguye anaaminika kuwa alijitoa muhanga mjini Paris.
No comments
Post a Comment