Zaidi ya abiria 300 wamenusurika baada ya moto kuwaka katika chumba cha injini ya meli ya Royal iliyokuwa ikitoka Unguja kwenda Pemba hii leo.
Taarifa kutoka visiwani Zanzibar zinasema kuwa, baada ya kutokea hitilafu hiyo ya moto, bahati nzuri meli ya Serengeti iliyokuwa inatokea Pemba kwenda Unguja ilipofika eneo la tukio ilitoa msaada ikiwa ni pamoja na kuwahamisha abiria toka meli hiyo ya Royal.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, wakati tukio hilo linatokea, meli hiyo ya Royal ilikuwa na abiria wapatao 374, watu wazima wakiwa ni 300 na watoto 74.
Abiria wakipatiwa msaada wa kuokolewa kutoka meli ya Royal kuhamishiwa Mv Serengeti |
Meli ya Royal ikivutwa na meli ya Mv Serengeti |
No comments
Post a Comment