Rais wa Niger, Mahamadou Issoufou, ametangaza kuwa jaribio la
mapinduzi ya kijeshi dhidi ya serikali yake limezimwa nchini humo.
Rais wa Niger amesema wanajeshi waliopanga njama za kuipindua
serikali yake wamekamatwa na watafikishwa mbele ya vyombo husika vya
sheria.
Habari zinasema kuwa, jeshi la wanahewa ndilo lililohusika zaidi kwenye jaribio hilo na tayari majenerali kadhaa wa kitengi hicho cha wanajeshi wametiwa mbaroni.
Polisi ya Niger imesema imemkamata Jenerali Salou Souleymane pamoja na Kanali Dan Haoua wa kitengo cha jeshi la anga kwa tuhuma za kupanga njama ya kuipindua serikali.
Mapinduzi ya kijeshi si jambo geni katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Mwaka 2010, jeshi lilimpindua rais wa wakati huo, Mamadou Tandja baada ya kushambulia ikulu ya rais Februari 18.
Hali ya wasiwasi imezidi kutanda nchini Niger huku uchaguzi mkuu wa mwezi Februari mwakani ukikaribia.

No comments
Post a Comment