Kikosi cha makomando wa Marekani kilichoenda nchini Libya siku
chache zilizopita kuimarisha uhusiano na mawasiliano na jeshi la
nchi hiyo kimedhalilishwa na kutimuliwa nchini humo.
Amesema makomando hao walilazimika kuondoka Libya muda mfupi baada ya kuwasili, baada ya kutakiwa kufanya hivyo na kundi moja la waasi katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Kikosi hicho cha makomando wa Marekani kilienda Libya mnamo Disemba 14, kwa kile kilichotajwa kuwa ‘kuimarisha uhusiano wa kiulinzi na kiusalama na jeshi la nchi hiyo’, lakini wakalazimika kuondoka kufuatia vitisho vya kundi la waasi katika nchi hiyo ya Kiafrika.
No comments
Post a Comment