Israel na Uturuki zimefikia makubaliano ya awali na kufufua uhusiano wa kidiplomasia, afisa wa Israel amesema.
Chini ya maafikiano ya sasa, Israel itafidia familia za waliouawa, nayo Uturuki iondoe madai yote dhidi ya Israel, afisa huyo amesema.
Hakujakuwa na thibitisho lolote rasmi kutoka kwa pande zote kwa sasa.
Makubaliano hayo yanadaiwa kufikiwa kwenye mkutano kati ya maafisa wakuu wa Usrael na Uturuki nchini Uswizi.
Kwa mujibu wa afisa huyo, ambaye jina lake halikutajwa, mataifa hayo pia yatabadilishana mabalozi.
Mazungumzo pia yataanza kujadili kuwekwa ka bomba la kusafirisha gesi kutoka Israel hadi Uturuki, afisa huyo ameongeza.
Uturuki kwa sasa inazozana na Urusi baada ya kudungua ndege ya Urusi.
Israel na Uturuki zilikuwa marafiki hadi Israel iliposhambulia meli hizo zilizokuwa zikisafirisha misaada kwenda Gaza, zikikiuka agizo la Israel la meli kutoingia Gaza.
No comments
Post a Comment