Rais wa Rwanda Paul Kagame |
Raia wa Rwanda wameanza kufika
vituoni kushiriki kwenye kura ya maoni ya marekebisho ya katiba, ambayo
yakiidhinishwa yatamruhusu Rais Paul Kagame kuwania urais kwa muhula wa
tatu.
Mabadiliko hayo yakiidhinishwa, huenda yakamuwezesha Bw Kagame kusalia madarakani hadi 2034.
Marekani imetoa wito kwa Bw Kagame kuonyesha uzalendo na kuondoka madarakani muda wake ukimalizika mwaka 2017.
Lakini kiongozi huyo ameyashambulia mataifa yanayotoa wito huo, akisema yanaingilia maswala ya ndani ya taifa hilo la Afrika Mashariki.
Mwezi uliopita, Bunge la Seneti nchini Rwanda liliidhinisha marekebisho hayo na kupisha kuandaliwa kwa kura ya maoni.
Bw Kagame atakuwa radhi kuwania urais kwa muhula mwingine wa miaka 2017 marekebisho yakiidhinishwa.
Hata ingawa marekebisho hayo yanapunguza muda wa muhula wa rais kutoka miaka saba hadi miaka mitano, na kudumisha muda wa mihula miwili, sheria hiyo haitaanza kutekelezwa hadi mwaka 2024.
No comments
Post a Comment