TAHARUKI imezuka katika kijiji cha Lusisi Wilayani
Wanging'ombe mkoani Njombe baada ya mwananuke mmoja kumtuhumu mumewe
kuwatoa msukule watoto wake kitu kilicho ibua hisia za wakazi wa kijiji
hicho na kufurika katika nyumba za familia hiyo.
Tukio hilo limetokea juzi kijijini hapo baada ya Lubeni
Mgaya kutuhumiwa kuwauwa kwa njia za kishurikina watoto wake wawili na
kuwafanya Misukule tuhuma zilizo tolewa na mkewe ailye fahamika kwa jina
la Anna Kilipamwambu na kusababisha watu kujaa kutaka kushuhudia
misukule hiyo.
Jeshi la pilisi mkoani Njombe baada ya kupata taarifa hizo
lilipiga kambi katika kijiji hicho ili kujiridhisha na tuhuma hizo
zilizo mwangukia mwanaume kutoka kwa mkewe.
Akizungumzia uchunguzi uliofanywa na jeshi hilo kamanda wa
polisi mkoa wa Njombe Wilbroard Mutafungwa amesema kuwa jeshi hilo
limebaini kuwa watoto wanao daiwa kuwa walikufa na kuchukuliwa misukule
kutoka kwa familia hiyo walikufa vifo vya kawaida kwa kuwa waliugua na
hatimaye kufariki.
Hivyo kamanda wa polisi ametoa wito kwa wakazi wa mkoa wa
Njombe kuachana na kufuatilia masuala ya kishirikina na kuwa kipindi
hiki ni msimu wa kilimo hivyo wajikite kwenye kilimo kwa maendeleo yao.
Mwandishi: John Banda
mhariri: Denice J Kazenzele
february 11/2016 [Alhamis]
No comments
Post a Comment