Yanga na Azam FC, zote zikiwa zimecheza Mechi 19, zina Pointi 46 kila mmoja lakini Yanga yupo Nambari Wani kwa Ubora wa Magoli kwa Kufunga Goli 44, Kufungwa 9, Tofauti ya Mabao ni 35 wakati Azam FC Kufunga 34, Kufungwa 11 Tofauti 23.
Kwenye Mechi ya kwanza ya VPL Msimu huu, Yanga na Azam FC zilitoka Sare ya Bao 1-1 hapo Oktoba 17.
Akizungumzia kuhusu Mechi yao hii, Kocha wa Yanga kutoka Uholanzi, Hans van der Pluijm, ambae Kikosi chake kimejichimbia Kambini huko Visiwani Pemba, amesema Mechi ni ngumu lakini wao wamejitayarisha kwa ushindi tu.
Pluijm alieleza: “Ni mchezo mgumu kwa Timu zote mbili, lakini hatuna budi kupambana kupata ushindi utakaotupatia nguvu kuelekea kutetea ubingwa wetu, lakini pia kuwafuata APR, tukiwa na matumaini ya ushindi kutokana na kikosi kuwa na ari ya kufanya vizuri,”
Mara baada ya Mechi hii na Azam FC, Jumatano ijayo Yanga watapaa kwenda Kigali, Rwanda kupambana na APR ya Rwanda katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Kwanza ya CAF CHAMPIONZ LIGI.
Nayo Timu inayoshika Nafasi ya 3 kwenye VPL, Simba, ambao wamecheza Mechi 20 na wana Pointi 45, Jumapili wapo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kuivaa Mbeya City ambayo ipo Nafasi ya 10 ikiwa na Pointi 21 kwa Mechi 20.
No comments
Post a Comment