Leicester wanaongoza Ligi wakiwa Pointi 3 mbele ya Timu ya Pili Spurs, waliotwaa Ubingwa mara ya mwisho Mwaka1961, na wa 3 ni Arsenal ambao mara ya mwisho kuwa Mabingwa ni 2004.
Hapa katikati wamepiga Dabi nyingi kati yao lakini hakuna hata moja iliyokuwa na nafasi kwa Mahasimu hao wa kuweza kutwaa Ubingwa kama hii.
Wachezaji wa timu na hali zao
Kipa wa Arsenal Petr Cech ataikosa Dabi hii baada ya kuumia Juzi kwenye Mechi na Swansea na atabadiliwa na David Ospina.
Pia Arsenal itamkosa Sentahafu Laurent ambae ameumia Musuli za Mguuni.
Baada ya kuzikosa Mechi 2, Kiungo wa Tottenham Mousa Dembele amepona Nyonga na atarejea Uwanjani.
kauli za makocha
Meneja Tottenham - Mauricio Pochettino: "Tunatarajia Gemu ngumu na tunahita nguvu kushinda Mechi hii”
-Meneja Arsenal Arsene Wenger: - "Ni moja ya Dabi chache ambayo Ubingwa unagombewa. Ni kubwa, na muhimu mno”
baadhi ya mechi walizokutana
-Tottenham wamepoteza Mechi 1 tu kati ya 7 zilizopita wakiwa kwao White Hart Lane dhidi ya Arsenal Wakishinda 4 Sare 2
-Arsenal walishinda Mechi ya mwisho Uwanjani White Hart Lane Mwezi Septemba kwenye Kombe la Ligi, Capital One Cup.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
TOTTENHAM
Hugo Lloris ,Kyle Walker ,Danny Rose ,Toby Alderweireld ,Kevin Wimmer ,Ryan Mason ,Erik Lamela,
Eric Dier,Dele Alli,Christian Eriksen, Harry Kane
Arsenal: David Ospina Per Mertesacker Gabriel Paulista Nacho Monreal Hector Bellerin Mesut Oezil Aaron Ramsey Alexis Sanchez Danny Welbeck Francis Coquelin Olivier Giroud
REFA: Michael Oliver
MECHI NYINGINE ZA EPL LEO
18:00: Chelsea ? - ? Stoke City
18:00 :Everton ? - ? West Ham United
18:00: Manchester City ? - ? Aston Villa
18:00: Newcastle United ? - ? AFC Bournemouth
18:00: Southampton ? - ? Sunderland
18:00: Swansea City ? - ? Norwich City
20:30: Watford ? - ? Leicester City
MECHI ZA KESHO EPL
16:30 Crystal Palace v Liverpool
19:00 West Brom v Man United
MSIMAMO WA LIGI {EPL} HADI SASA {KABLA YA MECHI HIZO}
No comments
Post a Comment