Barcelona imevunja rekodi iliyodumu miaka 27 nchini Hispania baada ya kucheza mechi 35 mfululizo bila kupoteza mchezo kwenye mashindano yote msimu huu hiyo ni baada ya kuichapa Rayo Vallecano kwenye mchezo wa usiku wa March 3 kuamkia March 4.
Leo Messi alipiga hat-trick kwenye mchezo huo baada ya wenyeji ya kukubali kipigo cha magoli 5-1 huku goli la kwanza likifungwa na Ivan Rakitic kutokana na makosa ya mlinda mlango wa Rayo.
Diego Llorente alitolewa nje kwa kadi nyekundu wakati Messi tayari ameshafunga magoli mawili kabla ya Manucho hajaiungia bao timu yake.
Manuel Iturra baadaye nae akatolewa nje kwa kadi nyekundu, Luis Suarez alikosa mkwaju wa penati ambao uliokolewa huku Messi akipachika bao la nne na kukamilisha hat-trick yake kwenye mchezo wa jana na Arda Turan akafunga bao la tano.
Goli la Arda Turan lilikuwa ni goli la kwanza kwa mchezaji huyo tangu ajiunge na Barcelona akitokea Atletico Madrid majira ya kiangazi ya msimu uliopita.
Kikosi cha Luis Enrique sasa kimetulia kileleni mwa La Liga kwa tofauti ya point inane na timu ambayo ipo nafasi ya pili ambayo ni Atletico Madrid.
Tazama magoli yote hapa>>>
No comments
Post a Comment