{Maoni Binafsi}
“watumbue
tu kama inawezekana pia wapasue kabisaaa, ili tuipate Tanzania yetu na sio Tanzania
ya wakoloni {ukoloni mamboleo}”
“Hivi
ikiwa viongozi wakishindwa kusimamia nafasi zao Rais anafanya nini zaidi ya
kujiuzulu? na ikiwa si kujiuzulu sio bora kuzifanya kazi yeye mwenyewe?”
“nchi
hii ikiwa katika mahangaiko kwa wananchi wake kuishi chini ya dola moja wakati
ambao tajiri mmoja mlo wake mmoja tu unafikia hadi zaidi ya shilingi elfu 50
hii ni kufuru”
Nashindwa kuwaelewa wanadamu hasa wanasiasa na wanaowafuata, maana wakati mtu akiharibu humuita dhaifu, mtuhumiwa, mwoga, mzito katika maamuzi, Mzigo n.k... lakini pia akiwa mwepesi kuchukua maamuzi huitwa mkurupukaji, mvunja katiba, asiyejua majukumu yake n.k.
Hivi ikiwa viongozi wakishindwa kusimamia nafasi zao
Rais anafanya nini zaidi ya kujiuzulu? na ikiwa si kujiuzulu sio bora kuzifanya
kazi yeye kwa kuwasimamisha wapotovu na kuwachagua wanaoweza kuendana na
kinachotakiwa na watanzania walio na uchungu na nchi yao? sasa mi nashangaa
siku hizi kuna watu waliojiita wanamapinduzi, wanaharakati na pengine
tungewaita wanamabadiliko tunawashuhudia wakibadilika na kuwa wana haki za
kibinadamu kwa kuwatetea wakosaji kisa wanataka kuonesha Rais ana mapungufu
katika hatua zake anazozichukua.
Mi nadhani kwa mtazamo wangu, kwa kiwango zaidi ya
changu cha kufikiri,na upeo wa wenye akili na uelewa wa kuchanganua mambo ni
bora kupata maendeleo kwa kila mtanzania tena ya haki kwa kuwaumiza walio
wachache lakini sio kuwaneemesha wachache isivyo haki kwa kuwaumiza walio
wengi...
Ni bora Rais JPM akakubali maneno yasiyo yenye
weledi kutoka kwa wasioona kinachotakiwa kwa wakati huu, ayasikilize lakini
katika utendaji aendelee na mipango yake yenye kuitafuta Tanzania yenye NEEMA
kwa watanzania wote.
Na kutoa fedha kwenye wizara moja na kupeleka kwenye
wizara nyingine wapo wanaodai sio kazi ya rais, sasa swali ni kwamba mbona
kikiharibika kitu analaumiwa rais? na ni nani mwenye kazi hiyo ikiwa wenye kazi
hiyo katika awamu zilizopita walishindwa kufanya kazi yao na kusababisha athari
zilizokuwa mtaji kwa wapinzani kuiangusha serikali.
Mi nadhani umefika wakati wa wapinzani wa serikali
kukubaliana na serikali kufanya kazi moja ambayo ni kuwasaidia wananchi kwa
kuisaidia serikali kufikia malengo chanya ambayo ndio sababu kubwa ya kuwepo
kwa upinzani licha ya kwamba natambua hakuna uwezekano wa kukubaliana na hili
kwa asilimia mia moja lakini tunaweza kujaribu tukiweza tuipitishe na
tukishindwa tukubali tumeshindwa na kuangalia mengineyo.
Kuna mambo mengi ambayo rais amelalamikiwa ikiwa ni
pamoja na {utumbuaji wa jipu} kusimamishwa kazi Meya wa jiji la Dar es salaam Wilson Kabwe
wakidai kavunja haki za binadamu kwa kumtumbua hadharani...Khaaa!! ulitaka iwe
siri wakati kila kitu kinajulikana kilichokuwa kikitokea nah ii ni kwa mujibu
wa hotuba ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaa katika siku ya Uzinduzi wa daraja la
Mwalimu Nyerere mwezi huu.
Nachoweza kusema sasa ni kwamba alikosekana tu mtu
wa kumtumbua,, lakini wengine wanaona kuwa hata huyu aliyejitoa mhanga kwa
ajili ya watanzania bado wanamuona hana maana na anatakiwa kufuata sheria,
sheria ipi inayokiukwa lakini wakati huo huo ilivunjwa na wengine nasi kupiga
kelele kumhitaji mtu sahihi wa kulishughulikia?
Umefika sasa wakati wa kila mtu kusimamia kitengo
chake wakati huo huo akishindwa basi bosi wake akifanye kwa kuwajibika au
kuwajibishwa nah ii sasa ndio itajenga heshima zaidi katika taifa tajiri kwa
mali lakini maskini kwa matumizi.
Leo ni aibu kwa uongozi kutokana na uhuru
waliopatiwa wananchi na wanasiasa wakiwemo viongozi kutokana na usaliti
wanaofanya kwa wananchi kwa kutotimiza ahadi zao kwa wananchi lakini muda huo
huo wakishutumiwa kumiliki mali za watanzania kinyume cha sheria huku nchi hii
ikiwa katika mahangaiko kwa wananchi wake kuishi chini ya dola moja wakati
ambao tajiri mmoja mlo wake mmoja tu unafikia hadi zaidi ya shilingi elfu 50
hii ni kufuru na matusi kwa watanzania wa kipato cha chini.
Huu sasa ni muda wa Rais JPM kuhakikisha mazoea na
dharau za viongozi anaviondoa ikiwezekana kwa kuvunja katiba ya nchi maana
itafikia hata mahakimu na majaji wanahitajika kutumbuliwa sasa hapa
pasipokutumia katiba isiyo rasmi atashindwa kwa hiyo ni lazima kupindisha
sheria ili kuokoa kinachotaka kupotea au kilichopotea tayari….
Rais John Pombe Joseph Magufuli, ni ombi langu kama
inawezekana lipitishe, kama ukiona haliwezekani tafadhali ni bora ulazimishe
wanyonge wa mali tajiri wa mawazo wako nyuma yako kukusaidia kuwamaliza wote
walio kinyume na kasi yako, watumbue tu kama inawezekana pia wapasue kabisaaa,
ili tuipate Tanzania yetu na sio Tanzania ya wakoloni {ukoloni mamboleo}
Wakati mwingine amekuwa akilazimishwa kutenda
kinyume cha sheria kwa sababu mambo hayo yanaonekana kuwawia vigumu kukamilisha
adhima yao, mfano ni mgogoro wa kisiasa Zanzibar, Rais JPM alipolazimishwa
kutoa maamuzi juu ya vurugu zile angali wakijua kabisa hana mamlaka hiyo
kisheria na imeandikwa katika sheria ya nchi hii kwa mujibu wa Mwenyekiti wa
tume ya uchaguzi Jaji Damian Lubuva lakini pi aMh. Mwenyewe aliwahi kugusia
suala hilo baada ya kubanwa akaamua kulitolea ufafanuzi.
Hitimisho: ifike wakati kila mtu afanye kazi yake,
lakini akishindwa siyo lazima aseme lakini msimamizi wake amwajibishe na
akishindwa pia nae awajibishwe na wananchi wenyewe, lakini sio sawa kumtuhumu
rais kwa mapambano aliyonayo maana kesho pia tutakuja kulalamika juu ya
unyanyasaji,wizi na matukio mengineyo dhidi ya viongozi wetu wasio waadilifu
kwa umma.
“Asante
kwa kupat anafasi katika ukurasa huu kuelezea haya”.
No comments
Post a Comment