Hatimaye Rais wa Serikali ya Mapunduzi ya Zanzibar ametangaza Baraza lake la Mawaziri akiwemo Hamad Rashid kutoka Chama cha Upinzani cha ADC.
Hamad Rashid Mohamed aliwahi kuwa mwanachama machachari wa Chama cha Upinzani, CUF kilichosusia uchaguzi wa marudio kwa madai kuwa kiliporwa ushindi katika uchaguzi wa awali uliofanyika mwezi Oktoba mwaka 2015.
Hamad Rashid alifukuzwa katika CUF akagombea Urais kwa Tiketi ya Chama cha Alliance for Democratic Change na kuambulia nafasi ya pili.
Hata hivyo hakufikia asilimia 10 ya kura zote ili apate nafasi ya kuwa makamu wa kwanza wa rais kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar iliyopatikana baada ya mvutano mkubwa kati ya Chama cha CUF na CCM.
Hii ndio Orodha ya baraza hilo la mawaziri:
- 1-ISSA HAJI USI GAVU-OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI.
- 2-HAROUNA ALI SULEIMAN-OFISI YA RAISI KATIBA,SHERIA,UTUMISHI WA UMMA.
- 3-HAJI OMAR KHERI-OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ.
- 4-MOHAMED ABOUD-OFISI YA MAKAMO WA PILI YA RAISI.
- 5-DR.KHALID SALUM MOHAMED-WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO.
- 6-MAHMOUD THABIT KOMBO-WAZIRI WA AFYA.
- 7-RIZIKI PEMBE-WAZIRI WA ELIMU.
- 8-AMINA SALUM ALLY-WAZIRI WA VIWANDA NA MASOKO
- 9-ALI KARUME-WAZIRI WA UJENZI,MAWASILIANO NA UCHUKUZI.
- 10-HAMAD RASHID-WAZIRI WA KILIMO MALIASILI MIFUNGO NA UVUVI.
- 11-RASHID ALI JUMA-WAZIRI WA HABARI, UTALII,UTAMADUNI NA MICHEZO
- 12-NURDIN KASTIKO-WAZIRI WA UWEZESHAJI,WAZEE,WANAWAKE NA WATOTO
- 13-SALMA ABOUD TALIB-MAJI, ARDHI,NISHATI NA MAZINGIRA.
- MANAIBU WAZIRI:-
- 1-HAROUS SAID SULEIMAN-AFYA
- 2-JUMA KHAMIS MAALIM-KATIBA
- 3-CHUM KOMBO-HABARI
- 4-LULU MSHAM KHAMIS-KILIMO
- 5-JUMA MAKUNGU JUMA-ARDHI
- 6-MOHAMED AHMED SALUM-UJENZI
- 7-MMANGA MJENGO MJAWIRI-ELIMU
No comments
Post a Comment