Watu wa Jamii ya Wawindaji, warina asali, na
waokota matunda pori kutoka kabila la Wahadzabe wanaoishi katika bonde la Yaeda
chini wilaya ya Mbulu wanakabiliwa na tatizo la njaa kali inayodaiwa kusababisha
baadhi ya wanaume kuzikimbia familia zao na kuiomba erikali na taasisi binafsi
zenye uwezo wa kusaidia kupatikana kwa chakula ziwasaidie kupunguza adha
hiyo.
Wakizungumza na ITV wazee wa jamii hiyo katika kijiji cha Mongoamono
wamesema hali imekuwa mbaya kwa upande wao na watoto ambao ndiyo waathirika
wakuu na inadaiwa imesababishwa na mabadiliko ya tabia nchi yanayochangiwa na
uharibifu wa mazingira unaofanywa na watu kutoka jamii nyingi na kwamba hawana
njia mbadala ya kupata chakula.
Kwa upande wao baadhi ya vijana wamesema hivi
sasa wanalazimika kuchimba mizizi hata isiyoliwa ili kuokoa uhai wao,watoto na
wazazi wao kwani hakuna matunda wala wanyamapori kama walivyozoea
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mongoamono Kata ya
Yaeda chini Bw. Pascal Kajema amesema uongozi umeanza kutoa elimu kwa jamii
hiyo ili kubadili mfumo wa maisha yao waweze kujihusisha na
shughuli zingine zikiwemo za kilimo ili kukabiliana na tatizo njaa.
No comments
Post a Comment