Wananchi wa kijiji cha Magunga wilayani Butiama
Mkoani mara wakishirikiana na baadhi ya wajumbe wa serikali ya kijiji
hicho,wamefanya maandamano kisha kuifunga kwa makufuli Ofisi ya Mwenyekiti wa
Serikali ya kijiji chao kwa madai kuwa uongozi wa kijiji umeshindwa
kutoa taarifa za mapato na matumizi katika kipindi zaidi Mwaka mmoja sasa.
Wakizungumza baada ya kuifunga Ofisi hizo za
Serikali ya kijiji hicho,wananchi hao wamesema mbali kijiji hicho
kukusanya mamilioni ya shilingi kutoka katika vyanzo mbalimbali zikiwemo
fedha za michango ya kutoka kwa wananchi, lakini uongozi wa Serikali ya
kijiji umeshindwa kutoa taarifa hizo za mapato na matumizi huku ukidaiwa
kutumia baadhi ya askari wa jeshi la Polisi kuwakamata na
kuwafungulia kesi wananchi wanajitokeza kuhoji matumizi ya mabaya ya fedha
hizo za kijiji.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw.Togoro
Juma,amekiri Ofisi hiyo kufungwa bila ya kufuatwa kwa taratibu na kwamba uongozi wa Serikali ya kijiji hicho umeshindwa kutoa taarifa hiyo
ya mapato na matumizi kwa madai ya kukosa muda mzuri wa kufanya
hivyo pia baadhi ya wananchi kuwa sehemu ya kikwazo kwa jambo hilo.
No comments
Post a Comment