Wananchi wa kata za
Bujugo na Kishogo zilizoko mkoani Kagera wamekumbana na athari za mvua
zinazoendelea kunyesha mfululizo mkoani huo kwa kukosa Mawasiliano ya usafiri
baada ya kivuko cha serikali cha Kyanyabasa ambacho husafirisha abiria na
mizigo kati ya kata hizo kupitia mto Ngono kukwama baada ya kamba ambazo
uongoza na kulinda usalama wa kivuko hicho kunaswa na Tingatinga
iliyosafirishwa na mkondo wa maji ya mvua.
Kutokana na athari
hiyo wananchi katika kata za Kishogo na Bujugo kwasasa kuvuka mto Ngono kutoka
sehemu moja kwenda nyingine wanatumia usafiri wa mitumbwi midogo inayohatarisha
usalama wa maisha yao ambayo hutumiwa na wavuvi kuvua samaki ndani ya mto huo
yenye uwezo wa kubeba abiria mmoja mmoja, kufuatia hali hiyo baadhi ya
wananchi wamesema kwa sasa wanasafirishwa kwa shilingi 500
badala ya shilingi 200 hivyo wameiomba serikali kutafuta uwezekano wa kujenda
daraja katika eneo hilo ili waweze kuondoka na usumbufu wanaoupata pale kivuko
hicho kinapopata hitilafu.
Itv
No comments
Post a Comment