Yanga ambayo ilifanikisha usajili huo jijini Dar es Salaam siku ya Jumatatu kwa dau la Sh30 mil, muda wa miaka miwili, ilifanya uchunguzi wa kina na kujikuta wakiokota dodo chini ya mgomba baada ya kumfuata mlezi wa mchezaji huyo, Halid Abdallah ambaye pia ni kiongozi wa TFF.
SINEMA ya kiraka, Juma Hassan Mahadhi aliyesajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili, ilikuwa bonge la picha. Mkanda uko hivi, kabla ya Mahadhi ambaye anaitwa Kiberenge kwa sababu ya kasi, nguvu awapo uwanjani kusaini Yanga, Simba ilikuwa miongoni mwa klabu iliyokuwa ikimwania kwa nguvu lakini wakateleza na kukosea kidogo, ndege akapeperuka.
Yanga ambayo ilifanikisha usajili huo jijini Dar es Salaam siku ya Jumatatu kwa dau la Sh30 mil, muda wa miaka miwili, ilifanya uchunguzi wa kina na kujikuta wakiokota dodo chini mgomba baada ya kumfuata mlezi wa mchezaji huyo, Halid Abdallah ambaye pia ni kiongozi wa TFF.
Lakini Simba wao, walipoteleza ni hapa, walipita njia ya mkato kumfuata mchezaji mwenyewe, tena wakiwa nyuma ya muda wakimtumia mmoja wa kiongozi wa klabu hiyo (jina tunalo) aliyemtaka mchezaji huyo apande basi kutoka Tanga hadi Dar es Salaam wakafanye mazungumzo.
Mahadhi, ambaye ni mjomba wa mchezaji wa zamani wa Yanga, Waziri Mahadhi na anatumia ubini wa Mahadhi upande wa mama yake na jina kamili la baba yake ni Hassan Chite anaeleza mkasa mzima hadi kutua kwake kwa watoto hao wa Jangwani.
“Ni kweli kabisa Simba walinihitaji, lakini mwisho wa siku ndiyo ikawa hivyo. Walichokifanya Yanga, walimaliza mambo na Mzee Halid, ambaye kwangu ndiyo mlezi na kila kitu. Simba wao walinifuata moja kwa moja na nilipolifikisha ujumbe kwake ndiyo ikawa hivyo,”anasema Mahadhi.
Mzee Halid ndiye amefanya safari yake ya soka ifike hapo alipo sasa, ndiye alimpangishia nyumba ya kuishi, anajua anakula nini na anaishi vipi pamoja na familia yake, akimpatia pesa za matumizi.
“Na wakati nafanya mazungumzo na yule kiongozi, Simba waliwatumia watu wawili tofauti kunitumia pesa ambazo ningezitumia kwa nauli ya kutoka Tanga hadi Dar es Salaam. Namba ya kwanza, ilituma sh 30,000 na ya pili 100,000. Zile thelathini kwa sababu zilikuwa na jina, nilifanikiwa kuzirudisha, lakini zile 100,000 ziliingia bila jina kwa namba ya wakala, nimeshindwa kuzirudisha, lakini kama nitamjua, nitazirudisha tu.”
SABABU YA KUSAINI YANGA
“Kwanza ni maslahi kama unavyojua mimi ni mchezaji, mpira ni ajira na ndiyo maisha yangu, pili nimefuata changamoto kwa sababu ni timu kubwa na ina wachezaji wenye uwezo wa juu ambao, kutokana uwepo wao nitafanikisha malengo yangu,” anasema Mahadhi na kufafanua namna atakavyokabiliana na changamoto ya namba kikosini hapo.
“Maisha ni mwenyewe, unachokipanda ndicho utakachovuna na kwenda Yanga, nitacheza na nakusisitizia, nitakuwa mzuri zaidi ya hivi nilivyo sasa kikubwa ni kujitambua na kutambua kilichonipeleka pale kwa kufanya mazoezi na nidhamu na kama kocha mwenyewe (Hans Pluijm) alinipendekeza hakuna shida.
“Na ninachokisisitiza, ipo siku utanikumbusha kauli yangu hii kuwa, nitakuwa mzuri zaidi ya unavyonijua. Kucheza na watu kama, Niyonzima (Haruna), Ngoma (Donaldo) na wengine wa kigeni, nitatoka tu. Nataka niitumie Yanga kufanikisha malengo yangu ya kwenda nje kucheza mpira wa mafanikio hasa Ulaya. Nafasi hiyo ipo na nitaipata kwa sababu ninacheza mashindano ya makubwa ya kimataifa na huko ndiko nitakapoonekana,” anasema Mahadhi anayeweka wazi, sababu amesaini Yanga, sasa mapenzi yake ni Yanga na atapambana kwa ajili ya timu hiyo.
Akiwa kwenye kikosi cha Coastal, Mahadhi alikuwa anavaa jezi namba nane ambayo katika kikosi cha Yanga, inatumiwa na Niyonzima, anasema: “Kweli jezi namba nane ndiyo roho yangu, inaniumiza sana na kama ningeipata, ningecheza kwa uhuru na amani, lakini kwa sababu pale Yanga ina mtu, inabidi niwe mpole, nitavaa jezi yoyote nitakayopewa.”
No comments
Post a Comment