WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema sukari haitakuwa tatizo katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na wakuu wa mikoa wamepewa maelekezo kilo moja isizidi Sh 2,300.
Alisema hayo jana wakati wa mahojiano na waandishi wa habari baada ya uzinduzi wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano uliofanyika Chuo cha Mipango mjini hapa.
Waziri Mkuu Majaliwa alisema hadi Mei 13, mwaka huu walikuwa wamepokea tani nyingine 35,000 za sukari na haitakuwa tatizo kwa kuwa tayari jitihada kuwa serikali imefanya katika kushughulikia suala hilo.
Pia alisema sukari nyingine tani 11,000 imeshatoka na inasambazwa na nyingine tani 20,000 iko tayari Tanzania na tani nyingine 35,000 zinakuja kabla ya Juni 30, mwaka huu.
Alisema sukari wameigawa kwa kanda kutokana na kanda kutofautiana kulingana na wingi wa watu kwa mujibu wa mgawo wa Bodi ya Sukari Tanzania wamepeleka maeneo yote.
“Niwasihi Waislamu wenzangu ambao wamefunga Ramadhani kwamba suala la sukari halitakuwa tatizo,” alisema.
“Mwito wangu kwa wafanyabiashara kuwa waaminifu na kutambua sukari ni mahitaji ya Watanzania wote.”
Alisema suala la bei wameangalia kule juu wanaponunua Brazil, Uarabuni na Malawi wameshaweka viwango vya bei ambavyo wakuu wa mikoa wataangalia sukari haitazidi Sh 2,300 kwa kilo ili Watanzania wote wamudu kununua.
Alitoa mwito kwa wafanyabiashara kuacha kuficha sukari kwani hayo ni mahitaji ya wananchi wote na hawana sababu ya kufanya hivyo.
Katika miezi ya karibuni, sukari ambayo ni moja ya bidhaa muhimu nchini, imepanda bei hadi kuuzwa kati ya Sh 2,500 hadi 3,000 kwa kilo kutoka Sh takriban 1,800, hali iliyosababisha serikali kuingilia kati kuwataka wafanyabiashara kuuza kilo moja kwa Sh 1,800 na kuagiza sukari kutoka nje ili kukabili upungufu uliopo.
Hizi hapa picha za matukio yote>>
|
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21 kwenye Ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma leo. Anayeshuhudia ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mapango, |
|
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango kitabu cha mpango huo. |
|
Mawaziri wakifurahi baada ya mpango huo kuzinduliwa. |
|
Waziri Mkuu, Majaliwa akimkabidhi mpango huo, Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson. |
|
Waziri Mkuu, Majaliwa akimkabidhi mpsngo huo Mbunge wa Jimbo la Korogwe kwa niaba ya Kiongozi Kambi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe ambaye ahakuwepo katika sherehe hiyo. |
|
Waziri Mkuu, Majaliwa akiwa na viongozi wote waliokabidhiwa mpango huo. |
|
Baadhi ya wazee na viongozi wa dini wakishiriki katika sherehe hizo |
|
Philip Mpango akijadiliana jambo na Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage |
|
Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Augustino Mahiga akizungumza na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. |
|
Profesa Jumanne Maghembe na Balozi Mahiga wakifurahia jambo |
|
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola akizungumza na Mahiga |
|
Dk. Mpango akimkaribisha Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson |
|
Naibu Spika akisalimiana na Mbuu wa Wilaya ya Dodoma mjini, Jasmine Tisekwa |
|
Naibu Sika akizungumza na Nape pamoja na January Makamba |
|
Waziri Mwijage akisalimiana na mmoja wa maofisa wa Wizara ya Fedha na Mipango |
|
Waziri Mkuu, Majaliwa akikaribishwa na Dk. Mpango |
|
Waziri Mkuu Majaliwa akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Fedha na Mipango, Doroth Mwanyika |
|
Baadhi ya wageni waalikwa |
|
Dk. Mpango akiteta jambo na Waziri Mkuu Majaliwa |
|
Kiongozi wa Dini ya Kiislamu akiomba dua ili mpango huo ufanikiwe |
|
Kiongozi wa Dini ya Kikristo akiuombea mpango huo |
|
Mawaziri wakiuombea mpango huo |
|
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana akitoa salamu za mkoa kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Majaliwa |
|
Kikundi cha ngoma za asili ya kabila la Wagogo cha Nyati kikitumbuiza |
|
Majaliwa akiwa namawaziri |
|
Waziri Mkuu, Majaliwa akiaga baada ya kuzindua mpango huo muhimu kwa Taifa |
No comments
Post a Comment