Video inayoonesha kauli hiyo ambayo imekuwa ‘viral’ katika mitandao ya kijamii ina mameno ya kuumiza ambayo yamewafanya wasanii wa filamu na mashabiki wa filamu kuisambaza zaidi katika mitandao ya kijamii.
Katika video hiyo Kanumba alisema “Nilikuwa na interview mbalimbali na watu mbalimbali kule South Africa, lakini wengi walikuwa wananiambia hivi kwenu watakuwa proud kiasi gani juu wako? Lakini kumbe hawakujua huku ninavyosemwa, wengine wamerekodi hata matangazo ya kunitukana mimi, kwa ajili ya kunidhalilisha, lakini nashukuru na namuachia Mungu, naipenda Tanzania ni nchi yangu, na nitaendelea kuipenda na nitaendelea kufanya kila niwezalo kwa nafasi yangu kupromote nchi yangu, kupromote sanaa yangu popote pale nilipo, pengine hata mchango wangu usipoonekana leo, basi hata nikishakufa utaonekana, pengine udongo na miti vitasema,”
Chanzo cha uhakika kilimtafuta mtayarishaji mkongwe wa filamu nchini, Mussa Banzi na kuelezea jinsi tukio hilo ambavyo lilimuumiza marehemu Steven Kanumba pamoja na sababu kuongea maneno hayo.
“Kweli hii video hata mimi nimeiona na nimesikitika sana,” alisema Mussa Banzi. “Mimi nakumbuka maneno yale aliongea siku chache baada ya kurudi Afrika Kusini, sasa Kanumba naye mwanzoni hakuwa mzuri kwenye lugha ya kingereza, sasa kukawa na clip ya video ambayo ilikuwa inasambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha akibabaika kuongea kingereza, watu waliitumia ile clip kumkejeli, wengine kama anavyosema mwenyewe waliandaa mabango ya kumkeji akifika airport. Kwa hiyo hali kama ile haikumpendeza kabisa, ndo maana alikuwa anaongea kwa uchungu sana,”
No comments
Post a Comment