Na Ezekiel Kamanga,Songwe
MKUU wa mkoa wa
Songwe Luten mtaafu Chiku Gallawa,kwa kushirikiana na kamati yake ya
ulinzi na usalama mkoani humo,amebuni mbinu mpya ya kuhakikisha mkoa huo
unakuwa kati ahali ya usafi kwa kuanza kufanya usafi wa mazingira kwa
kila halmashauri kwa kushirikisha viongozi wa wilaya zote ambapo zoezi
hilo litakuwa endelevu kila mwisho wa mwezi.
Mwezi
huu mwishoni mwa wiki,viongozi hao kutoka kila halmashauri wakiongozwa
na Mkuu wa Mkoa walikuwa kwenye halmashauri ya mji wa Tunduma ambapo
walifanya usafi kwa kushirikiana pamoja na madiwani na wananchi maeneo
yote ambapo mwezi ujao watafanya usafi kama huo katika halmashauri ya
wilaya ya Mbozi na kulifanya zoezi hilo kuwa endelevu kwa kila mwezi
kusafisha halmahsuri moja
Akizungumza mwishoni mwa
wiki na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa usafi
huo,Gallawa,alisema licha ya kutii agizo la Rais John Pombe Magufuri,la
kufanya usafi kila juma mosi ya mwisho wa mwezi,lakina aliona atumie
mbinu mbadala itakayorahisisha shughuri hizo kufanyika kwa weredi zaidi
kwa kushirikiana .
Alisema katika mpango huo,wa
kufanya usafi kwa kushirikiana aliona aanze na halmashauri ya mji wa
Tunduma kwa kuwa ndiyo unaozarisha kwa kasi taka ngumu kutokana na kuwa
na idadi kubwa ya watu wanaofanya shughuri mbalimbali katika maeneo yote
ambapo aliweza kutoa maelekezo kwa wakazi wa mji huo kuwa jukumu la
kutunza taka ni lao ambapo wanatakiwa wazitoe nje pindi gari la taka
linapopita.
Gallawa,alisema baada ya kukamilisha
usafi katika mji wa Tunduma pamoja na kuweka utaratibu wa watu kutunza
taka majumbani mwao alisema zoezi hilo liwe endelevu kwa wakazi wa eneo
hilo kuhakikisha wanatunza hali ya usafi ambapo viongozi wa halmahsuri
wanatakiwa kutembelea maeneo yote kujionea hali ya usafi na kuwachukulia
hatua za kisheria watakao kaidi agizo au utaratibu huo.
Alisema
mwezi ujao watafanya shughuri kama hizo kwenye halmashauri ya wilaya ya
Mbozi na ambapo wakiwa huko wakikamilisha usafi watapanga mwezi
unaofuata waende halmahsuri gani na kuwa lengo ni kuhakikisha mkoa wa
Songwe unakuwa ni wa mfano kwa usafi na kuwa baada ya hapo utawekwa
utaratibu wa kila sekta kuwa na maeneo maalum ya kufanyia kazi.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya nji wa Tunduma,Herode Jivava,alipongeza mpango huo na
kusema kuwa watasimamia kwa ufasaha mpango huo licha ya kuwepo na
changamoto ya uhaba wa magari ya kuzolea taka ambapo alisema kwa mwaka
2017- 2018 katika bajeti ijayo halmashauri hiyo itakuwa imenunua magari
ya kubebea taka ambapo alisema watakuwa na uhakiki mji wa Tunduma
utaendeleo kuwa msafi.
Mkuu wa wilaya ya Momba Juma
Ilando,alisema mpango wa serikali ni mzuri hasa walipoanza kusafisa
katika mji wa Tunduma ambao upo kwenye wilaya yake na kuahidi kuendeleza
ushirikiano huo katika kazi hiyo kwa halmahsuri zingine na kuwa Tunduma
kitaifa ilishika nafasi ya tatu kwa usafi na kupewa tuzo ambapo mwaka
ujao alisema anataka iwe ya kwanza na kuzipiku halmahsuri za Moshi na
Katavi zilizoibuka kidedea kwa usafi mwaka 2016.
Wananchi
wa upande wao wamepongeza hatua hiyo na kusema kuwa watatoa ushirikiano
wa kutosha kuhakikisha mazingira yote yanakuwa katika hali ya usafi
ambapo walitumia nafasi hiyo kuiomba serikali ipeleke magari ya kubeba
taka utokana na halmashuri hiyo kuzarisha taka nyingi ambazo wengi wao
wamekuwa wakitupa pembezoni mwa barabara ombi ambalo lilipokelewa na
serikali.
No comments
Post a Comment