CONTE BADO MTAMU TU, CRYSTAL PALACE WAKALIA KIMOJA KWAO USUKANI KAMA KAWA
Akifunga bao lake la 50, straika wa Chelsea, Diego Costa ameiwezesha timu yake hiyo kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Crystal Palace na kuwa ushindi wa 11 mfululizo katika Premier msimu huu, hivyo kujitengenezea mazingira mazuri ya kuwa mabingwa wa ligi hiyo.
Ushindi huo umeifanya Chelsea inayonolewa na Antonio Conte kuendelea kujikita kileleni ambapo sasa imefikisha pointi 9 dhidi ya yule anayeshika nafasi ya pili.
Diego Costa alifunga bao hilo katika dakika ya 43 akiunganisha kwa kichwa mpira uliopigwa na beki wake wa pembeni, Cesar Azpilicueta.
Katika mchezo huo, kiungo wa Chelsea, N'Golo Kante na Costa walipata kadi za njano ambazo ni za tano kwa kila mmoja na hivyo kutakiwa kuukoa mchezo ujao dhidi ya Bournemouth.
Kipingo hicho ni pigo kubwa kwa Crystal Palace kwa kuwa inahaha kukwepa mkiani katika msimamo ambapo inataka kukimbia kushuka daraja.
No comments
Post a Comment