Yanga imepaa hadi kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania bara mara baada ya ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya JKT Ruvu katika mchezo wa kwanza wa raundi ya pili.
Ushindi dhidi ya JKT Ruvu unaifanya Yanga ifikishe jumla ya pointi 36 baada ya kucheza mechi 16 pointi moja mbele ya mahasimu wao Simba ambao watacheza kesho dhidi ya Ndanda FC mchezo wao wa kwanza wa raundi ya pili ya VPL.
Yanga wamepata goli la kwanza la Yanga dakika ya 37 kipindi cha kwanza kufuatia krosi maridadi ya Saimon Msuva kuunganishwa kimiani na beki wa Ruvu Michael Aidan akiwa katika harakati za kuondoa hatari langoni kwakeMsuva akafunga bao la pili dakika ya 57 kabla ya kufunga tena dakika ya 90 na kuilaza JKT Ruvu huku Yanga ikikaa kileleni mwa ligi ikisubiri matokeo ya Simba.
Lwandamina amepata ushindi wa kwanza katika mechi yake ya kwanza VPL baada ya kupoteza mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu dhidi ya JKU ya Zanzibar.
Bakari Shime ‘Mchawi Mweusi’ amepoteza mechi yake ya kwanza VPL tangu alivyoachana na Mgambo JKT ya Tanga na kuchukuliwa na TFF kuifundisha timu ya taifa ya vijana wa U-17 ‘Serengeti Boys.’
Ilikuwa ni mechi ya kwanza kwa makocha wa timu zote ndani ya (Bakari Shime-JKT Ruvu na George Lwandamina-Yanga) Shime si mgeni wa VPL lakini amesimama kwa mara ya kwanza kama kocha wa JKT Ruvu wakati Lwandamina yeye ameisimamia Yanga kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa VPL.
Ushindi wa Yanga dhidi ya JKT Ruvu ni wa nane (8) mfululizo tangu mwaka 2013, timu hizo zimecheza michezo nane tangu mwaka 2013 na Yanga imeshinda mechi zake zote kwa zaidi ya magoli mawili.
KIUNGO mpya wa Yanga, Justin Zulu ameondolewa ghafla katika kikosi cha Yanga kinachocheza na JKT Ruvu jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kutokana na kutopata kibali cha kufanya kazi nchini.
Mapema jana Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilionya mchezaji ambaye hatakuwa na kibaki cha kufanya kazi nchini kutoka Idara ya Uhamiaji hatacheza na Yanga inakuwa ya kwanza kukumbana na kibano hicho.
REKODI
1. 17/12/2016 JKT Ruvu 0-3 Yanga
2. 26/10/2016 Yanga 4-0 JKT Ruvu
3. 07/02/2016 JKT Ruvu 0-4 Yanga
4. 19/09/2015 Yanga 4-1 JKT Ruvu
5. 25/03/2015 JKT Ruvu 1-3 Yanga
6. 05/10/2014 Yanga 2-1 JKT Ruvu
7. 06/04/ 2014 Yanga 5-1 JKT Ruvu
8. 01/11/2013 JKT Ruvu 0-4 Yanga
Yanga imeshaifunga JKT Ruvu jumla ya magoli 29 katika mechi nane zilizopita huku yenyewe ikiruhusu magoli manne tu tangu mwaka 2013.
WAFUNGAJI
Rn Player Name Timu Goal
1 Ramadhan Shiiza Kichuya Simba SC 9
2 Saimon Msuva Yanga SC 9
3 Amisi Tambwe Yanga SC 8
4 John Bocco Azam FC 7
5 Rashid Mandawa Mtibwa sugar 7
6 Donald Ngoma Yanga SC 6
7 Haruna Chanongo Mtibwa sugar 5
Msimamo Mpya wa Ligi Kuu Msimu Huu.
Rn
|
Timu
|
P
|
W
|
D
|
L
|
F
|
A
|
Gd
|
Pts
|
1
|
YANGA
|
16
|
11
|
3
|
2
|
34
|
8
|
26
|
36
|
2
|
SIMBA
SC
|
15
|
11
|
2
|
2
|
26
|
6
|
20
|
35
|
3
|
Azam
FC
|
15
|
7
|
4
|
4
|
23
|
14
|
9
|
25
|
4
|
KAGERA
SUGAR
|
16
|
7
|
4
|
5
|
16
|
16
|
0
|
25
|
5
|
MTIBWA
SUGAR
|
16
|
6
|
6
|
4
|
20
|
19
|
1
|
24
|
6
|
STAND
UNITED
|
15
|
5
|
7
|
3
|
15
|
12
|
3
|
22
|
7
|
Ruvu
Shooting
|
16
|
4
|
8
|
4
|
15
|
17
|
-2
|
20
|
8
|
MBEYA
CITY
|
16
|
5
|
5
|
6
|
13
|
15
|
-2
|
20
|
9
|
T.
PRISONS
|
15
|
4
|
7
|
4
|
9
|
10
|
-1
|
19
|
10
|
NDANDA
FC
|
15
|
5
|
4
|
6
|
13
|
16
|
-3
|
19
|
11
|
African
Lyon
|
15
|
4
|
5
|
6
|
10
|
15
|
-5
|
17
|
12
|
MWADUI
FC
|
16
|
4
|
4
|
8
|
13
|
21
|
-8
|
16
|
13
|
MAJIMAJI
FC
|
15
|
5
|
1
|
9
|
12
|
23
|
-11
|
16
|
14
|
Mbao
FC
|
15
|
4
|
3
|
8
|
15
|
20
|
-5
|
15
|
15
|
JKT
RUVU
|
16
|
2
|
7
|
7
|
6
|
15
|
-9
|
13
|
16
|
TOTO
AFRICANS
|
16
|
3
|
3
|
10
|
9
|
18
|
-9
|
12
|
Msimamo Kabla ya kuingia mzunguko wa pili vpl
Mechi za leo 2016-12-17
JKT RUVU 0-3 YANGA SC
RUVU SHOOTING 1-1 MTIBWA SUGAR
MBEYA CITY 0-0 KAGERA SUGAR
MWADUI FC 1-0 TOTO AFRICANS
MWADUI 1-0 TOTO AFRICAS
Mwadui FC wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 mbele ya wageni wao Toto Africans katika uwanja wa Mwadui Complex.
Katika mchezo huo wa leo Mwadui FC iliwabidi wasubiri mpaka dakika 70 kupata goli lao pekee kupitia kwa mtokea benchi Salim Khamisi na kufanikiwa kuwafunga goli 1-0 Toto Africans.
Katika mchezo mwingine uliochezwa katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya Kagera Sugar wamelazimisha sare kwa Mbeya City ya bila kufungana, huku ndugu zao Mtibwa Sugar wakitoa sare ya goli 1-1 na Ruvu shooting.
MICHEZO ZA KESHO DECEMBER 18
16:00 MBAO FC Vs STAND UNITED
16:00 NDANDA FC Vs SIMBA SC
16:00 African Lyon Vs Azam FC
16:00 T.PRISONS Vs MAJIMAJI
No comments
Post a Comment