Kwa sasa moja ya midahalo inayoendelea kwenye ulimwengu wa michezo ni kuhusu mshahara mpya wa Sanchez ambae labda anaweza ku sign mkataba mpya na Arsenal hivi karibuni kama wakikubaliana.
Sasa kitu cha msingi ambacho kitaamua mkataba huo bila shaka ni mshahara wake.
Tusizunguke sana kwa kusikiliza maneno ya kusema kwamba anapapenda Arsenal au hapapendi.
Kama angekua hapapendi angesha sepa.
Sasa kilichobaki ni uhakika wa pesa zitakazomridhisha na mkataba usainiwe.
Gazeti la The Sun limeandikwa kwamba Sanchez anataka pound laki tatu ili asaini mkataba mpya.
Habari hizo zimetoka leo zikiweka mkazo kwamba kutokana na dau la kutoka China linawapa jeuri watu wa Sanchez kudai mshahara mzuri kwa mchezaji wao.
Wiki iliyopita Sanchez alipokea ofa ya Pound laki tano kutoka timu ya China Super League ili ajiunge na ligi hiyo.
Mshahara huo ni mara mbili ya mshahara ambao labda atapewa na Arsenal ambao ni pound laki mbili na nusu.
Huu ni wakati mgumu kidogo kwa board ya Arsenal ambao ni maarufu kwa kutoa mshahara kidogo tofauti na timu nyingine kubwa.
Changamoto inakuja pale mchezaji kama Sanchez alivyo kwenye form nzuri kwa sasa.
Kucheza ni namna moj ana maslahi ni namna ya pili, sisi ni mashabiki ngoja tuone nini atakachoamua mwenye maamuzi.
Credit:Shaffihdauda.com
No comments
Post a Comment