Benki kuu ya Tanzania inapenda kuwafahamisha wananchi wote kuwa,habari inayoenea katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba noti ya shilingi mia tano haitatumika tena kuanzia Desemba 31,2016; sio taarifa ya kweli na ni uvumi unaopaswa kupuuzwa.
Ukweli ni kwamba noti ya shilingi 500 itaendelea kuwepo katika mzunguko sambamba na ile sarafu ya shilingi 500 hadi pale noti hiyo itakapotoweka mikononi mwa wananchi.
Tafadhali mpuuze taarifa hizo sio za ukweli.
Marcian Kobello. Mkurugenzi wa Huduma za kibenki- BoT .
No comments
Post a Comment