Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » JESHI LA POLISI LAKAMATA KUKAMATA NYARA ZA SERIKALI ZA THAMANI YA TSH MIL.81 NA WATUHUMIWA 121 WA MAKOSA MBALIMBALI
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

………………………………………..
JESHI la Polisi nchini kwa kushirikiana na Ofisi za Shirikisho la Polisi Duniani (Interpol) kanda ya Kusini mwa Afrika, imefanikiwa kukamata nyara za serikali zenye thamani ya Tsh. Milioni 81 na watuhumiwa 121 wa makosa mbalimbali.
 
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Alhamisi (Oktoba 1, 2015), Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi, Kamishna Diwani Athuman ,alisema kuwa lengo la operesheni hiyo ni kuongeza tija katika swala zima la kupambana na uhalifu.
 
“Lengo la operesheni hii ni kuongeza tija katika kupambana na hali ya uhalifu na kuweka mazingira salama kwa wananchi na nchi jirani” alisema Kamishina Athuman. 
 
Aidha aliongeza kuwa operesheni hiyo ilifanyika nchi nzima katika kanda nane ikiwemo kanda ya Kaskazini, kanda ya juu Kusini, kanda ya ziwa, kanda ya magharibi, kanda ya Zanzibar, kanda ya kati na kanda ya kusini na kufanikiwa kukamata vielelezo na watuhumiwa wa makosa mbalimbali.
 
Kamishani Athumani alisema kuwa vielelezo vilivyokamatwa katika operesheni hiyo ni pamoja na magari mawili yaliyoripotiwa kuibiwa nchini Japan na Afrika ya kusini ,dawa za kulevya, wahamihaji haramu 7, kutoka Kenya, Burundi na Msumbiji, bidhaa zilizopigwa marufuku zenye thamani ya Tsh. Milioni 3.5 na madini yenye thamani ya Tsh. Milioni 74.
 
Aliongeza kuwa watuhumiwa mbalimbali walikamatwa kwa kujihusisha na makosa ya kuhujumu miundo mbinu ya Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) na hatua za kisheria zitachukuliwa endapo watakutwa na hatia na kufikishwa mahakamani
 
Kamishina Athumani amewaomba wananchi kushirikiana na Jeshi la polisi kwa kutoa taarifa pale wanapoona tukio la uhalifu kutoka kwa mtu au kundi la watu likiingia nchini kinyume na sheria na pia kuwa makini wakati wanapoagiza magari kutoka nje kwa kuwasiliana na ofisi za Interpol za ndani na nchi husika ili kuepuka usumbufu wa kukamatwa na gari za wizi.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / JESHI LA POLISI LAKAMATA KUKAMATA NYARA ZA SERIKALI ZA THAMANI YA TSH MIL.81 NA WATUHUMIWA 121 WA MAKOSA MBALIMBALI

No comments :