Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » ASKOFU WA KANISA KATOLIKI JIMBO LA SHINYANGA ATEMA CHECHE..AYASHUKIA MATAIFA MAKUBWA...NA WANAOPUUZA AMANI YA TANZANIA
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Askofu wa jimbo katoliki la Shinyanga mhashamu Liberatus Sangu ameeleza kushangazwa na kusikitishwa na vitendo vya mataifa makubwa duniani kuhubiri amani duniani wakati wao ndiyo wana viwanda vikubwa vya kutengeneza silaha za kivita na kuuza ili watu waendelee kupigana matokeo yake kusababisha vifo,mateso na mahangaiko katika mataifa huku wahanga wakubwa wakiwa ni watoto,akina mama na wazee.

Askofu Sangau ameyasema hayo leo asubuhi katika adhimisho la misa takatifu ya Krismasi iliyofanyika katika kanisa kuu la Mama Mwenye Huruma la Ngokolo mjini Shinyanga.

Amesema wakati dunia inaadhimisha sikukuu ya Krismasi mataifa mengi hayana amani vita kutokana na baadhi watu kuwa na uchu wa madaraka na fedha.

“Mataifa makubwa yanayohubiri amani ndiyo wana viwanda vikubwa vya kutengeneza silaha, wanauza wapi? ili upate soko la silaha,lazima utengeneze vita,watu wapigane,ili bidhaa itoke,lakini ndiyo hao wanaokaa mezani na kusema wanataka amani,,nadhani hawajanuia kuleta amani,uchu wa madaraka na fedha ndicho kinachosumbua",ameeleza askofu Sangu.

"Tuwaombee wenzetu katika nchi zenye vita,mwenyezi mungu apate kuwajalia amani na utulivu ili sote kama familia ya watoto wa mungu tufike kule kristo ametutangulia”,ameongeza Askofu Sangu.

Katika hatua nyingine Askofu Sangu amewataka kuwapuuza watu wanaosema nchi ya Tanzania haina amani na kusisitiza kuwa Tanzania ni nchi yenye amani huku akiwataka watanzania kumwombea rais John Pombe Magufuli aliyeonesha nia ya kuwatumikia wananchi bila upendeleo na ameonesha wazi wazi kuwa ana mtanguliza mwenyezi mungu katika maisha yake.

“Kuna baadhi ya watu wanataka kutusadikisha kuwa Tanzania hakuna amani kwa nia zao wenyewe,labda wakilinganisha Tanzania na mbinguni ni sawa, kwa sababu mbinguni kuna utumilifu wake wote,lakini ukilinganisha Tanzania na mataifa mengine,ndugu zangu tuna amani ambayo tunapaswa kuilinda kwa nguvu zetu zote”,ameeleza Sangu.

Katika hatua nyingine amewashangaa wazazi na walezi wanaoruhusu watoto wao kwenda kwenye kumbi za starehe na kusisitiza kuwa familia yoyote bora kamwe haiwezi kuruhusu mtoto kwenda disko.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / ASKOFU WA KANISA KATOLIKI JIMBO LA SHINYANGA ATEMA CHECHE..AYASHUKIA MATAIFA MAKUBWA...NA WANAOPUUZA AMANI YA TANZANIA

No comments :