Na John Banda, Dodoma
.......................................
Mtu mmoja mkazi wa
Kizota Manispaa ya Dodoma amejinyonga mpaka kufa Baada ya Kudhani amemuua mama
yake mzazi kwa kumchoma visu mara 3 katika maeneo ya Tumboni, shingoni na
ubavuni siku ya Christmas.
Katika taarifa iliyotumwa
na jeshi la polisi kwa vyombo vya habari ilionyesha kuwa Des,25 mwaka huu
majira saa 12:00 jioni huko Kizota Mbuyuni Manispaa ya Dodoma, mtu mmoja
aitwaye TATU OMARI, miaka 74 alijeruhiwa kwa kuchomwa na kisu tumboni, shingoni
na ubavuni na mtoto wake aitwaye HAMISI ISSA, miaka 40.
Taaarifa Imesema mara
baada ya tukio hilo Issa alijifungia
chumbani kwake na kujinyonga hadi kufa akidhani amemuua mama yake huku
ikibainisha kuwa Chanzo chake ni ulevi wa pombe kupindukia.
Taarifa hiyo ilisema Matukio
mengine yaliyojiri katika kipindi cha sikukuu watu watatu wamekamatwa kwa
makosa ya kupatikana na Bhangi kinyume cha sheria ambapo SOPHIA PAUL [16],
mkazi wa eneo la Itega Manispaa ya Dodoma alikamatwa akiwa na misokoto 47 ya
bhangi, REGINADO MARIKI, miaka [27], mkazi wa kijiji cha Mpinga Wilaya ya Bahi
alikamatwa na mabunda 23 ya Bhangi MUSSA
AUGUSTIN MUHOGO alikamatwa akiwa na Bhangi misokoto 21.
Aidha EXAVERY JONAS MOGOPE, mia [23], mkazi wa
Chazungwa Mpwapwa akiwa na sare za Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambazo
ni Kofia aina ya pama, suruali na shati kombati kinyume cha sheria, sare
alizoiba baada ya kutoroka mafunzo RUVU JKT mwaka 2013. Watuhumiwa wote wamefikishwa
mahakamani jana.
Natoa shukrani kwa
Wananchi wote Wakazi wa Dodoma kwa kutambua kwamba usalama unaanzia majumbani
mwao na kusherehekea sikukuu za Maulid na Christimass kwa Amani na utulivu.
Ninatoa wito waendeleze utamaduni huo katika kipindi cha sherehe za kuaga mwaka
2015 na kuukaribisha mwaka mpya 2016.
Pia watambue watakao shindwa kutii sheria
bila shuruti wakamatwe na kufikishwa makamani.
No comments
Post a Comment