Jaribio la dawa mpya nchini Ufaransa limemwacha mtu mmoja akiwa hana fahamu huku wengine watano wakiwa katika hali mbaya.
Jaribio hilo lilifanywa na mahabara ya kibinafsi katika mji wa mgaharibi wa Rennes.
Kufikia sasa Jaribio hilo limesimamishwa na kwamba kampuni hiyo imeanza kuwarudisha watu waliojitolea.Haijajulikani ni watu wangapi waliohusishwa.
Ripoti za vyombo vya habari kwamba dawa hiyo iilitengezwa kutokana na bangi zimepingwa na wizara ya afya.
Afisi ya mwendesha mashtaka mjini Paris imesema kuwa uchunguzi umeanzishwa
Waziri wa afya Marisol Touraine ,ambaye alikuwa akielekea Rennes siku ya ijumaa ,aliahidi kujua ukweli kuhusu swala hilo lililosababisha ajali hiyo.
Jaribio hilo lilifanywa na Biotrial,kampuni moja ya Ufaransa ilio na sifa ya kimataifa kwa kufanikiwa majaribio chungu nzima tangu ilipoanzishwa mwaka 1989.
Kulingana na wizara ya afya,ajali hiyo ilitokea siku ya alhamisi.Athari kubwa ni kukosa fahamu kwa mwathiriwa mmoja ,ilisema huku wengine watano wakiwa katika hali mbaya sana.
Utafiti huo ni wa awamu ya kwanza ambapo watu waliojitolea hutumia dawa hiyo ili kubaini usalama wake,wizara hiyo ilisema.
No comments
Post a Comment