Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » MKUU WA MKOA ATAKA WALIMU WAPYA WAPANGWE DODOMA VIJIJINI
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Na Peter Mkwavila Dodoma.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa amewaagiza Maafisa elimu kuwapanga walimu wapya maeneo ya vijijini ili kukabiliana na tatizo la uhaba lililopo katika maeneo hayo.

Akizungumza juzi Mjini hapa katika kikao cha kazi cha watendaji wa sekta ya elimu ngazi ya Halmashauri,Mkuu huyo alisema shule za vijijini zimekuwa na upungufu wa walimu hivyo kuwataka maafisa elimu kuwapanga walimu wapya katika maeneo hayo.

‘’Shule za pembezoni zimekuwa na upungufu wa walimu,walimu wapya wamekuwa wakipangwa shule za mjini ama za barabarani,wakati kuna baadhi ya shule za mjini zinaziada ya walimu nawaomba maafisa elimu wote kutatua tatizo hilo’’alisema

Alisema tatizo lingine ni walimu kuhamishwa kutoka shule zenye upungufu kwenda zenye walimu wa kutosha na mahali pengine kwenye ziada halia mabayo imekuwa ikichangia kushuka kwa elimu.

Pia alisema Halmashauri ya Dodoma ndiyo inaongoza kwa upangaji mbaya wa walimu kwani kuna shule zenye wanafunzi 500 huku walimu wakiwa ni watatu. 

Alisema kwa miaka mitatu mfulilizo mkoa wa Dodoma umefanya vibaya katika matokeo ya darasa la saba pamoja na kidato cha nne hivyo kuwataka wanaohusika na elimu kulishughulikia suala hilo.

‘’Majukumu yanayopaswa kuzingatiwa mwaka 2016 ni kuhakikisha walimu wote wanafundisha kikamilifu,ukaguzi na ufuatiliaji vifanywe kwa wakati na kuhakikisha shule zetu zinatoa elimu bure’’alisema Gallawa.

Kwa upande wake Afisa Elimu wa Mkoa wa Dodoma Juma Kaponda alitoa majukumu kwa walimu kufikiri,kupanga na kutekeleza kila kinachowezekana ili kuinua taaluma katika Mkoa wa Dodoma.

Pia aliwataka kusimamia utekelezaji wa elimu bure na kuchukua hatua kwa yeyote anayekiuka maagizo hayo.

‘’Niwaombe tuwahamasishe wazazi kuchangia chakula cha mchana kwa shule za kutwa na milo yote kwa shule za kutwa zenye hostel’’alisema

###############mwisho######################

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / MKUU WA MKOA ATAKA WALIMU WAPYA WAPANGWE DODOMA VIJIJINI

No comments :