Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » WANAANDAMANA KUMFUATA MKUU WA MKOA WA DODOMA...KISA NINI KIJUE HAPA
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Na John Banda, Dodoma

WAKULIMA zaidi ya 400 wa kata ya kikuyu kusini wamesema wanaanza na maandamano kumfuata mkuu wa mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa na kama hakitaeleweka watapiga hodi kwa Lukuvi Kumshitaki Mtendaji wa kata yao Kikuyu kusini Juma Mainda anayetaka kukwamisha zoezi la umilikishwaji wa viwanja vyao vilivyokwishapimwa na CDA.

Wakiongea katika mlima wa Image kata ya Kikuyu kusini manispaa ya Dodoma  kuliko na viwanja hivyo wakulima hao walisema kitendo cha Kiongozi huyo pamoja na wenzake kutaka kuivunja kamati ya mashamba na kusababisha zoezi la umilikishwaji wa viwanja vyao vilivyopimwa tangu mwaka jana kusimama ni sawa na kuwaombea umasikini.

Kwa upande wake katibu wa kamati ya mashamba Javan Majen alisema jumla ya wakulima 450  ambao wamekuwa wakilima kwa kipindi kirefu Mashamba katika kata ya kikuyu kusini ikiwemo mlima wa image mpaka sasa wanasota wasijue cha kufanya kuhusu umilikishwaji wa viwanja vyao ambavyo vilipimwa na CDA Tangu mwaka jana.

Katibu huyo alisema wakulima zaidi ya 400 walipimiwa viwanja zaidi ya 2000 toka kwenye mashamba yao na kuahidiwa kila mtu kupewa umiliki wa viwanja sawa na ukubwa wa shamba lake lakini sasa kuna kizungumkuti kutokana na zoezi hilo kuingiliwa na Afsa Mtendaji dakika za mwisho na kusababisha lisimame.

Majeni  Alisema upimaji huo uliofanyika mwaka 2015  chini ya usimamizi wa kamati ya watu 10 ya wenye mashamba iliyoteuliwa na wao wenyewe huku viongozi wote wa mtaa na kata wakiwa kwenye kamati nyingine iliyokuwa inasimamia Upimaji wa Nyumba, Mapagale pamoja na misingi.

Alisema tangu wapimiwe viwanja hivyo mpaka sasa Bado swala la umilikishwaji limesimama kutokana na kile alichoita kuingiliwa na viongozi wa kata na mtaa ambao wamekua wakitaka zoezi la uhakiki lifanyike upya huku likisimamiwa na wao badala ya kamati ya mashamba

“Hapa kikuyu kusini kuna kamati mbili moja ni ya mashamba ambayo imekuwa ikifuatilia upimaji tangu mwaka 2014 ilipoundwa lakini pia kuna nyingine ya Nyumba, mapagale na misingi na zote ziliundwa ili kufuatilia haki za wananchi CDA lakini sasa tunashangaa kuingiliwa kwa kamati yetu.

Tuna uhakika kuwa Diwani, Mtendaji wa kata pamoja na wenyeviti wa mitaa wanataka kuipunguza nguvu kamati hii kwa ajili ya masrahi yao binafsi, maana ukiangalia mbona sisi tuliteseka mpaka kufikia kupimiwa  kwanini leo, hatutakubali wahakiki kwa kuwa hawamjui hata mtu mmoja mwenye shamba.

Sasa sisi hatutakubali tutahakikisha tunapita ngazi zote hata kama kumuona waziri mkuu kama tutanyimwa haki ngazi za chini na hivi karibuni kama tutaona hakieleweki tunaomba kibali cha maandamano ya amani kueleke kwa mkuu wa mkoa wetu kuomba usaidizi”, alisema

Akijibu tuhuma hizo Afsa Mtendaji wa Kata ya Kikuyu Kusini Juma Mainda kwa njia ya simu alisema anashangazwa na maswala hayo kutangazwa kwenye vyombo vya habari na hata hivyo yeye siyo msemaji atafute mkurugenzi wa manispaa nje ya hapo mwandishi afike ofisini kwake akaonyeshwe mikataba ya mradi huo wa upimaji

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / WANAANDAMANA KUMFUATA MKUU WA MKOA WA DODOMA...KISA NINI KIJUE HAPA

No comments :