Na Peter Mkwavila.....Dodoma
VIJANA wanaosoma vyuo vikuu wameshauriwa kuwakumbuka watu
wenye mahitaji maalumu katika kuwapatia misaada mbalimbali badala ya kuelekeza
kwenye mambo ya anasa.
Ushauri huo umetolewa na jana,Mjini hapa na
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Chuo cha Mipango(IRDP)
Veronica Mwembezi wakati alipokuwa wakikabidhi misaada mbalimbali kwa watoto
wanaoishi katika mazingira hatarishi wa kituo cha Upendo Miyuji.
Aliitaja misaada iliyotolewa na jumuiya hiyo ya
wanawake ni pamoja na vyakula vikiwemo unga wa kula,sukari,mchele,mafuta ya
kula na nguo vyote vikigharimu zaidi ya laki tano..
Alisema jamii ya watu wenye mahitaji maalumu
wanachangamoto nyingi zikiwemo za kiafya na kielimu ambazo vijana wasomi wa
vyuo vikuu wanaweza kuzitatua kwa kujitoa kifedha na kimali pia.
“Lakini cha kusikitisha leo hii vijana hao wasomi
walio wengi wapo tayari kujitoa kwenye burudani ya mambo ya anasa,badala ya
kuelekeza kwa watu hao wenye mahitaji maalumu kama vile watoto wanaoishi katika
mazingira magumu,yatima,wajane, wazee na wale wanaoishi na viruzi vya ukimwi”alisema.
Hata hivyo kwa upande wa serikali pia imetakiwa kuongeza
nguvu kwa taaisisi mbalimbali zinazojishughulisha na kuwasaidia jamii ya watu
wenye mahitaji hayo.
Kwa upande wake msimamizi wa kituo hicho ya watoto Br
Getachew ameviomba vyuo vikuu vingine kuviangalia vituo hivyo vya kulelea
watoto kwa jicho la huruma kutokana na hali mbaya iliyopo ya uendeshaji.
Alisema kuwa kwa asilimia kubwa ya vituo vyenye
mahitaji maalumu vimekuwa vikikabiliana
na changamoto ya ukosefu wa misaada mbalimbali ikiwemo kwa upande wa elimu afya
na hata kwenye mavazi pia.
No comments
Post a Comment