Na John Banda
VIONGOZI wa dini halmashauri ya
wilaya ya Njombe wameombwa kushiriki kikamilifu katika kamati za
Kupambana na ukimwi zitakazo undwa na halmashauri hiyo kwa kutoa ushauri
ili kupambana na maambukizi ya ugonywa huo ambao mkoa wa Njombe wa
ujumla unaonekana kinala kw akuwa wamaambukizi.
Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya
ya Njombe Valentono Hongoli wakati akizungumza na wadau wa maendeleo wa
halmashauri hiyo juzi ambao walikutana katika mkutano wa maendeleo ya
halmashauri.
Amesema kuwa viongozi wa dini wasisite kujumuika na
wataalamu na madiwani wa halmashauri hiyo watakapo wekwa katika kamati
za halmashauri hiyo hasa ile ya ukimwi kwa kutoa usahauri.
Amesema kuwa kanuni za baraza la madiwani wa halmashauri
hiyo zinataka katika mamati ya ukimwi kuwepo kwa viongozi wa dini
kwaajili ya ushauri hivyo viongozi hao mchango wao unahitajika sana
katika kamati zao.
Hata hivyo kamati hizo zitaundwa hivi karibuni na kuwepo
kwa kiongozi mmoja kutoka kwa taasisi ya Kiislamu na mmoja kutoka
taasisi ya Kikristo.
Hongoli ameongeza kuwa kuna baadhi ya watu wanadaiwa kuacha
kutumia dawa za kupunguza makali na kuacha matumizi ya dawa hizo na
kusema kuwa kwa busala za viongozi wa dini kunaweza kuwashawishi
viongozi wa dini wanaweza kurudi kutumia dawa.
Aidha mkutano huo ulichukua mda mfupi kujadili mambo ya
kimaendeleo ya halmashauri hiyo ambapo kulijumuishwa wadau wa maendeleo
wakiwembo viongozi kutoka taasisi mbalimbali, viongozi wa dini na
wataalam wa halmashari hiyo.
No comments
Post a Comment